• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Wasioamini Mungu wataka kila familia iwe na mtoto mmoja

Wasioamini Mungu wataka kila familia iwe na mtoto mmoja

NA WINNIE ONYANDO

CHAMA cha Wasioamini Mungu nchini kimetoa wito kwa serikali kuanzisha sera itakayomlazimisha mtu kuzaa mtoto mmoja ili kudhibiti idadi ya watu nchini.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Rais wa chama hicho, Harrison Mumia, alisema kuwa sheria hiyo itanufaisha vizazi vijavyo kwa kupunguza ushindani wa kazi jambo analodai litaboresha sekta ya ajira nchini.

“Kupungua kwa idadi ya watu nchini kutafanya watu wasishindane hasa wakati wa kutafuta kazi,” Mumia alisema.

“Tunaitaka serikali ya Rais William Ruto kutekeleza sera hiyo ili kila familia iwe na mtoto mmoja ili kudhibiti idadi ya watu nchini. Sera ya mtoto mmoja itatoa manufaa mengi kwa vizazi vijavyo, kijamii na kiuchumi.”

Kadhalika, Bw Mumia alidai kuwa tafiti zinaonyesha kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, na kwa hivyo, kutekeleza sera hiyo kusaidia katika kudhibiti ongezeko la watu nchini.

Kando na hayo, chama hicho kinataka idadi ya watu idhibitiwe ili kupambana na umaskini nchini.

Bw Mumia amewahi kufanya kazi ya masuala ya kidijitali katika Benki Kuu ya Kenya (CBK).

  • Tags

You can share this post!

Maonyesho ya ASK yasababisha upungufu wa maji Nairobi

Jinsi watalii wawili walivyopoteza mali ya thamani...

T L