• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 4:55 PM
Waziri Soipan Tuya apongezwa kwa kuomba kwa Kiswahili sanifu   

Waziri Soipan Tuya apongezwa kwa kuomba kwa Kiswahili sanifu   

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto Jumatano, Juni 7, 2023 anaongoza nchi katika maombi ya kitaifa.   

Sala hizo zinafanyika katika Mkahawa wa Kifahari wa Safaripark, Nairobi.

Waziri wa Mazingira na Misitu Bi Soipan Tuya ni mmoja wa viongozi wakuu serikali ya Dkt Ruto walioalikwa kuomba.

Huku akiwa mwanamke wa kwanza kutoka jamii ya Kimaasai kuwahi kuhudumu katika Baraza la Mawaziri Nchini, Bi Soipan alipongezwa kufuatia ufasaha wake wa Kiswahili katika sala.

“Kumbe mbali na kuwa hodari karika Kiingereza, wewe pia ni mweledi wa Kiswahili.

“Tumefurahia na kushukuru jinsi umetushirikisha kwenye maombi kwa lugha sanifu ya Swahili,” akamsifu Waziri mwenza Davis Chirchir, Kawi.

Bi Soipan, amewahi kuhudumu kama Mbunge Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Narok, kati ya 2013 – 2017.

Viongozi wengine wakuu na mashuhuri serikalini waliohudhuria hafla ya maombi Safaripark ni pamoja na Naibu Rais Bw Rigathi Gachagua, Mkuu wa Mawaziri Bw Musalia Mudavadi, maspika Moses Wetangula (bunge la kitaifa), Amason Kingi (seneti), miongoni mwa wengine.

  • Tags

You can share this post!

Mswada wa Fedha: Mikakati ya Azimio kuuzima imeiva

Rais Ruto aongoza Wakenya katika Maombi ya Kitaifa vinara...

T L