• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Aliyeanika nyaraka zinazoonyesha ‘Ruto si mtu wa kuaminika’ ashtakiwa

Aliyeanika nyaraka zinazoonyesha ‘Ruto si mtu wa kuaminika’ ashtakiwa

NA MASHIRIKA

WASHINGTON DC, AMERIKA

MFANYAKAZI wa kambi ya kijeshi ya Amerika Jack Teixeira, anayeshukiwa kutoa nyaraka za siri za Pentagon, alifikishwa mahakamani mjini Boston, Massachusetts.

Nyaraka hizo zilionyesha kuwa afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa (UN) alisema kuwa hamuamini Rais wa Kenya, Dkt William Ruto.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu. Teixeira alishtakiwa rasmi kwa kuchukua bila idhini na kumiliki hati na nyenzo zilizoainishwa.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwanasheria Mkuu wa Amerika, Merrick Garland, amemtaja kama mfanyakazi katika jeshi la angani la Amerika na kiongozi wa kundi la mtandaoni ambako hati hizo zilifichuliwa kwa mara ya kwanza.

Kukamatwa kwa Teixeira kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa wiki nzima uliochochewa na ripoti katika vyombo vya habari vya Amerika kuhusu mojawapo ya uvujaji mbaya zaidi wa taarifa za siri tangu sakata ya Edward Snowden mwaka 2013.

Afisi ya jeshi la angani nchini Amerika, imesema kuwa Teixeira alijiunga na kikosi hicho mwaka 2019.

Wizara ya ulinzi ya Amerika, Pentagon ilikuwa imesema kuwa kuvuja kwa taarifa hizo kunatoa “hatari kubwa” kwa usalama wa taifa hilo lenye uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi duniani.

Kukamatwa kwa Teixeira kumetokea siku moja baada ya gazeti la “The Washington Post” kuripoti kuwa mamia ya kurasa za nyaraka zilikuwa zimewekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Discord na mtu ambaye alikuwa akifanya kazi katika kambi ya jeshi la Amerika.

  • Tags

You can share this post!

Ufaafu wa Oginde kuongoza EACC kuamuliwa Mombasa

Haji mjumbe aliyepatanisha Raila na Ruto

T L