• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
DPP aamuru Mkenya apelekwe Amerika kushtakiwa

DPP aamuru Mkenya apelekwe Amerika kushtakiwa

Na RICHARD MUNGUTI

NAIROBI, KENYA

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji ameomba mahakama iamuru mwanaume aliyeacha shule baada ya kuhitimu Darasa la Nane apelekwe Amerika kushtakiwa kwa ulaghai wa Sh1.1 bilioni.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani, Wendy Kagendo Michemi aliombwa aruhusu Abdulrahaman Imraan Juma almraafu Rahaman apelekwe Amerika kujibu mashtaka.

Bi Michemi alifahamishwa kuwa mshukiwa huyo alijifanya Mkurugenzi wa Benki nchini Amerika na kwamba angefadhili ujenzi wa shule ya kimataifa ya watoto waathirika wa vita ambao wazazi wao waliangamia kwa ugaidi.

Abdulrahaman, baba wa watoto watatu anadaiwa kulaghai raia wa Qatar pesa akimdanganya atajenga shule ya kimataifa ya kushughulikia watoto maskini na wale ambao wazazi wao waliangamizwa na vurugu za kijamii na ugaidi.

Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Bi Catherine Mwaniki kwamba mshukiwa huyo alihitimu elimu ya Darasa la Nane katika nchi jirani ya Uganda.

“Mshukiwa huyu alikuwa anakutana na mlalamishi na kumdanganya ameendelea na ujenzi huku akidai pesa zaidi. Pesa hizo zilikuwa zinatumwa katika akaunti ya benki yake nchini Kenya,” hakimu alifahamishwa.

  • Tags

You can share this post!

Wizara kufunza wakazi kilimo cha kibiashara

Vuguvugu la Umoja Mlimani lasambaratika

T L