• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 5:30 PM
Vuguvugu la Umoja Mlimani lasambaratika

Vuguvugu la Umoja Mlimani lasambaratika

ANITA CHEPKOECH na MERCY SIMIYU

VUGUVUGU la Umoja wa Mlima Kenya (MKUF) limesambaratika na sasa kila chama kitasimamisha wawaniaji wake katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Jana Ijumaa, chama cha The Service Party (TSP) kinachoongozwa na aliyekuwa waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri, kilisema kila chama kitasimamisha wawaniaji wake.

Vuguvugu la MKUF lilijumuisha kinara wa Narc Kenya Martha Karua, Moses Kuria (CCK) na Spika wa Bunge Justin Muturi wa Democratic Party (DP) na gavana wa zamani wa Kiambu William Kabogo ambaye ni kiongozi wa chama cha Tujibebe Wakenya.

You can share this post!

DPP aamuru Mkenya apelekwe Amerika kushtakiwa

Raila kupokea wabunge wa ANC Murang’a

T L