• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Jinsi mahakama nchini Nigeria ilivyoagiza jogoo msumbufu achinjwe

Jinsi mahakama nchini Nigeria ilivyoagiza jogoo msumbufu achinjwe

Na MASHIRIKA

HAKIMU wa mahakama moja Kaskazini mwa Nigeria alitoa hukumu ya kifo kwa jogoo mmoja aliyeshtakiwa kwa kuwakosesha majira utulivu.

Hakimu Mkuu wa mji wa Kano, Halima Wali, alitoa hukumu hiyo baada ya majirani wawili kuwasilisha kesi mbele yake wakilalamika kuwa jogoo huwakosesha usingizi kwa kuwika “usiku kucha, haswa alfajiri ambapo usingizi huwa mtamu.”

Walalamishi hao pia walisema jogoo huyo huwakosesha amani kila mara.

Mmoja wa walalamishi hao, Yusuf Mohammed, wa makazi ya Ja’en aliambia mahakama hiyo kwamba kuwika kwa jogoo huyo kila mara kunampokonya haki yake ya kulala.

Huku akikiri kuwa jogoo wake ni mwenye kelele nyingi, Isyaky Shu’aibu, mmiliki wa kuku huyo, aliomba mahakama hiyo isitishe utekelezaji wa hukumu hiyo.

Hata hivyo, hakimu alipuuzilia mbali ombi hilo baada ya kushawishiwa na walalamishi na kuamuru kwamba jogoo huyo afungiwe na kuchinjwa.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Meat pie

Ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba karibu na Ikulu

T L