• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
MAPISHI KIKWETU: Meat pie

MAPISHI KIKWETU: Meat pie

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa mapishi: Saa mbili

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • kilo mbili za nyama ya kitoweo, kata vipande vya inchi ¾
  • vijiko 2 vya chumvi
  • vijiko 3 vya mafuta ya mboga
  • vijiko 4 siagi isiyo na chumvi
  • vitunguu maji 2 vilivyokatwa vipande vyembamba
  • punje 4 za vitunguu saumu, kata vipande vipande
  • kikombe ¼ cha unga wa ngano
  • vikombe 2 vya mchuzi wa nyama (meat broth)
  • kijiko 1 cha nyanya ya kopo
  • vijiko 2 vya majani ya zaatari
  • kijiko cha poda ya vitunguu
  • kijiko ½ cha pilipili nyeusi
  • sosi ya Worcestershire
  • yai 1
  • karatasi ya kuokea keki
Nyama ikiiva kwenye mafuta yaliyopashwa kwa moto wa juu. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Koroa nyama pande zote na chumvi kiasi cha kijiko na nusu.

Pasha mafuta kwenye sufuria nzito juu ya moto mwingi. Mara tu mafuta yanapopata moto, weka nyama kwenye sufuria, ongeza nyama na upike, ukiipindua mara kwa mara hadi iwe na rangi ya hudhurungi pande zote. Itakuchukua muda wa dakika 10. Hamisha steki kwenye sahani.

Nyama baada ya kuchemshwa ndani ya mafuta katika sufuria nzito kweye moto wa juu. PICHA | MARGARET MAINA

Punguza moto uwe wa wastani na uongeza vijiko viwili vya siagi halafu usubiri mpaka iyeyuke. Ongeza vitunguu kwenye sufuria.

Funika na upike, ukichochea mara kwa mara, hadi vitunguu viive sana. Bila shaka itakuchukua muda wa dakika 10. Ongeza vitunguu na kaanga hadi viwe na harufu nzuri, kama dakika moja zaidi.

Koroga vijiko viwili vilivyobaki vya siagi hadi viyeyuke. Nyunyiza unga na kuchochea ili kuchanganya. Ongeza meat broth, nyanya ya kopo, zaatari, sosi ya Worcestershire, poda ya vitunguu, pilipili na chumvi nusu kijiko iliyobaki. Koroga ili kuchanganya vizuri.

Rudisha steki kwenye sufuria, pamoja na juisi yoyote iliyokusanyika. Ongeza moto uwe wa juu na uache nyama ya steki ichemke. Punguza moto kuwa mdogo, funika na upike hadi mchuzi uwe mzito na nyama ya ng’ombe iwe laini. Muda utakaotumika ni saa moja.

Washa ovena hadi joto la sentigredi 200. Weka mchanganyiko wa nyama ya ng’ombe kwenye sufuria ya pie au sahani ya kuoka. Paka yai kwenye chombo cha kuokea.

Weka kinyunya cha unga wa ngano kwenye chombo cha kuoka, ukifunika mchanganyiko wa nyama kabisa. Ukitumia kisu unda matundu kadhaa na uipake kwa juu yai iliyobakia.

Peleka pie kwenye ovena na uoke hadi uwe wa kahawia kama saa moja

Ondoa pie kutoka kwenye ovena na uiruhusu ipoe kwa muda wa baina ya dakika tano hadi 10 kabla ya kupakua na kufurahia.

  • Tags

You can share this post!

Hatua za kuchukua kuacha matumizi ya sukari nyingi

Jinsi mahakama nchini Nigeria ilivyoagiza jogoo msumbufu...

T L