• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 6:55 PM
Ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba karibu na Ikulu

Ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba karibu na Ikulu

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYABIASHARA mashuhuru Ashok Doshi pamoja na wakili mwenye tajriba ya juu Harith Sheth wameshtakiwa kwa ulaghai wa shamba karibu na Ikulu ya Nairobi.

Doshi alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina na kukanusha mashtaka manne ya kunyakua shamba hilo la thamani ya Sh2 bilioni, lake Jenniffer Nthenya Wambua.

Doshi alikana alikatalia katika shamba hilo lililoko Processional Way kaunti ya Nairobi na kuhatarisha amani.

Doshi, Sheth na kampuni ya Magnum Properties Limited walikabiliwa na shtaka kutengeneza risiti feki ya kulipa ushuru wa shamba hilo, la nambari LR209/3850 na kuipunja wizara ya ardhi ada ya Sh1.2 milioni.

Na wakati huo huo, Bw Onyina alimwamuruu Bw Sheth afike kortini kujibu mashtaka.

Bw Onyina alimwachilia Doshi kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh500, 000.

Pia kampuni ya Magnum iliagizwa ilipe dhamana ya Sh500, 000 itakayolipwa na Doshi.

Kesi itatajwa Mei 2, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi mahakama nchini Nigeria ilivyoagiza jogoo msumbufu...

Vyakula bora vya kusaidia kuimarisha umeng’enyaji wa...

T L