• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:12 PM
Mabilionea waangamia wakizuru meli iliyozama

Mabilionea waangamia wakizuru meli iliyozama

NA MASHIRIKA

SAFARI iliyokuwa ya furaha ya kutaka kubaini kilichozamisha meli ya kihistoria ya Titanic iliyozama miaka 110 iliyopita iligeuka kuwa janga.

Safari hiyo iliyoaminiwa kuwa salama, iliwahusisha mabilionea wanne pamoja na mwana wa mmoja wao, na ilianza Jumapili mwendo wa saa kumi na moja alfajiri, kabla ya kuishia kwa majonzi tele.

Nyambizi hiyo yenye urefu wa futi 21 iliyobandikwa jina Titan, ilinuia kuwapeleka watano hao kuona mabaki ya meli ya Titanic na kubaini kilichoizamisha.

Kulingana na Kikosi cha Coast Guards Amerika, nyambizi hiyo ilipoteza mawasiliano na meli iliyokuwa ikiisaidia, muda wa saa mbili baada ya kuanza safari katika Atlantiki ya Kaskazini Juni 18.

Waliokuwa kwenye nyambizi hiyo ni Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa OceanGate mwenye umri wa miaka 61, mfanyabiashara wa Uingereza na Pakistan Shahzada Dawood, 48, na mwanawe Suleman, 19, na mfanyabiashara wa Uingereza Hamish Harding, 58 pamoja na Paul-Henry Nargeolet,77, aliyekuwa mpigambizi wa zamani wa jeshi la wanamaji la Ufaransa.

(Kushoto-Kulia, juu kuenda chini) Hamish Harding, Afisa Mkuu Mtendaji wa OceanGate Expeditions Stockton Rush, Paul-Henri Nargeolet, na Suleman Dawood na babake Shahzada Dawood. Watano hao inaaminika “kwa masikitiko wameangamia.” PICHA | AFP

Kulingana na shangazi ya Suleman, mwana huyo alikuwa na uoga wa kuendelea na safari hiyo, ila baadaye akabadili msimamo.

“Dawood ambaye alikuwa kwenye chombo hicho pamoja na babake, mfanyabiashara Shahzada Dawood, alikuwa na hofu ya kuendelea na safari hiyo. Hata hivyo, alikubali kwenda na baba yake ili kusherehekea Siku ya Baba,” akasema shangaziye Suleman.

Vifusi vilivyopatikana wakati wa msako wa chombo hicho, vinaonyesha kuwa huenda nyambizi hiyo ilipata ajali mbaya baada ya kufika karibu na vifusi vya meli hiyo ya kihistoria ya Titanic.

“Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa marafiki na wapendwa wa watano hao,” akasema afisa John Mauger.

Kampuni ya OceanGate Expeditions, inayomiliki nyambizi hiyo, ilisema katika taarifa kwamba watu wote watano waliokuwa ndani, wamekufa.

Baadhi ya nchi zilizohusika katika mchakato wa kutafuta vifusi vya nyambizi na miili ya waathiriwa wa Titan ni Canada, Amerika, Uingereza na Ufaransa.

Kikosi cha Coast Guards, kilidokeza Alhamisi kuwa usakaji wa vifusi vya chombo hicho utakuwa mgumu kutokana na presha ya maji.

  • Tags

You can share this post!

Kocha Rafael Benitez apokezwa mikoba ya kunoa Celta Vigo ya...

Kindiki atekeleza mabadiliko tata ya kiutawala...

T L