• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Kocha Rafael Benitez apokezwa mikoba ya kunoa Celta Vigo ya Uhispania

Kocha Rafael Benitez apokezwa mikoba ya kunoa Celta Vigo ya Uhispania

Na MASHIRIKA

MKUFUNZI wa zamani wa Liverpool na Newcastle United, Rafael Benitez, amerejea katika ulingo wa ukocha baada ya kukubali mikoba ya Celta Vigo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Kocha huyo raia wa Uhispania amekuwa nje ya ulingo wa ukocha tangu Januari 2022 alipopigwa kalamu na Everton.

Benitez, ambaye pia aliwahi kushikilia mikoba ya ukocha kambini mwa Chelsea, amekubali mkataba wa miaka mitatu ya kunoa Celta.

Anajaza nafasi ya kocha Carlos Carvalhal aliyeagana na Celta mwishoni mwa msimu wa 2022-23 baada ya kusaidia kikosi hicho kukwepa shoka ambalo vinginevyo lingewateremsha ngazi kutoka La Liga.

Celta walikamilisha kampeni za La Liga kwa alama tatu juu ya vikosi vilivyoteremshwa daraja baada ya kukamata nafasi ya 13. Walitandika mabingwa Barcelona katika siku ya mwisho ya kampeni.

Benitez aliwahi pia kuwa mkufunzi wa Inter Milan, Real Madrid na Napoli. Aliwahi kuongoza Liverpool kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2005 na Kombe la FA mnamo 2006. Chelsea walishinda taji la Europa League mnamo 2013 wakiwa chini ya Benitez ambaye pia aliwahi kuongoza Newcastle kupanda ngazi kutoka Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mapinduzi ndani ya Jubilee ni haramu – Kioni

Mabilionea waangamia wakizuru meli iliyozama

T L