• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
‘Maradona alifariki kutokana na utepetevu na mapuuza ya madaktari’

‘Maradona alifariki kutokana na utepetevu na mapuuza ya madaktari’

Na AFP

SAN ISIDRO, Argentina

MWANASOKA mashuhuri wa Argentina, Diego Maradona, alifariki kutokana na mapuuza ya madaktari, wakili wa muuguzi anayechunguzwa kuhusiana na kifo hicho amesema.

“Walimuua Diego,” wakili Rodolfo Bague aliwaambia wanahabari Jumatano baada ya mteja wake, muuguzi Dahiana Gisela kuhojiwa na waendesha mashtaka.

Maradona alifariki kutokana na tatizo la mshtuko wa moyo mnamo Novemba 2020 akiwa na umri wa miaka 60.

Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo kutokana na tatizo la kuganda kwa damu.

Muuguzi mwenye umri wa miaka 36 ni mmoja wa watu saba wanaochungwa kwa kosa la mauaji bila kukusudia. Hii ni baada ya kundi la wataalamu waliokuwa wakichunguza kifo cha Maradona kubaini kuwa hakupewa matunzo ya kutosha “baada ya kutelekezwa na madaktari”.

Lakini wakili Bague alisisitiza kuwa ni madaktari waliokuwa wakimtibu Maradona wala sio mteja wake.

Alisema ni madaktari hao waliopaswa kulaumiwa kwa kifo cha mwanasoka huyo wa zamani wa Argentina.

Alisema Maradona alikuwa akitibiwa kwa tatizo la moyo japo kwa upande mwingine alikuwa akitumia dawa za kutibu matatizo ya kiakili ambazo ziliongeza mapigo ya moyo.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Ukraine yakomoa Macedonia Kaskazini na kusajili ushindi wa...

Kevin de Bruyne atambisha Ubelgiji dhidi ya Denmark kwenye...