• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 1:01 PM
Mchecheto NATO ikituhumu China kusaidia Urusi kuipiga Ukraine

Mchecheto NATO ikituhumu China kusaidia Urusi kuipiga Ukraine

NA MASHIRIKA

LUZHNIKI, MOSCOW

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa NATO anahofia China inasaidia Urusi kushambulia Ukraine.

Akiongea mnamo Jumatano, Jens Stoltenberg amesema muungano huo wa kijeshi umeona baadhi ya ishara kwamba China inaweza kuwa inapanga kuiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Aidha, Stoltenberg ameitaka Beijing kuachana na kile ambacho amesema, kitakuwa ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Isitoshe, akizungumza na Shirika la Habari la AP katika mahojiano Stoltenberg alisema kwamba muungano huo, ingawa haushiriki katika vita, utaiunga mkono Ukraine “kwa muda mrefu utakaohitajika.”

Wakiendela na mahojiano alipoulizwa iwapo NATO ina ushahidi wowote kwamba China inaweza kuwa tayari kutoa silaha au msaada mwingine kwa vita vya Urusi, Stoltenberg alisema kuna ishara za kuonyesha hivyo. Mbali na hayo, aliongeza kwamba nchi kama vile Marekani ambayo ni moja kati ya washirika wa NATO imekuwa ikionya China kuhusu kusaidia nchi ya Urusi.

“Tumeona baadhi ya ishara kwamba wanaweza kupanga hilo na bila shaka washirika wa NATO, Marekani, wamekuwa wakionya dhidi ya hilo kwa sababu ni jambo ambalo halipaswi kutokea. China haipaswi kuunga mkono vita haramu vya Russia,” akasema.

Katika Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) uliofanyika Jumamosi, iliyopita Jens Stoltenberg alizua wasiwasi, akihusisha mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine na China.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, “Kinachotokea Ulaya leo,” alionya,”kinaweza kutokea Asia kesho,” ambayo wengi wanaamini kuwa ni dokezo la wasiwasi kuhusu vita katika kisiwa cha Taiwan.

Kama kiongozi wa kisiasa wa Marekani, NATO inatimiza matakwa ya Marekani.

Pia katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alidai kuwa China kuiunga mkono Urusi katika mzozo huo kutachipuza uchokozi.

Bali na hayo Maadhimisho ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine yatakuwa kesho Ijumaa.

Mapema wiki hii, Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Marekani Joe Biden walitoa hotuba za hali ya juu wiki hii ambapo walikosoa nchi za kila mmoja wao na kubadilishana maneno juu ya mzozo huo.

Rais Putin alilaumu nchi za Magharibi kwa vita vya Ukraine wakati wa hotuba ya Jimbo la Muungano siku ya Jumanne.

Kando na hayo, katika hafla nyingine ya kuunga mkono vita iliyofanyika mnamo Jumatano, rais aliongoza umati wa watu kwa nyimbo za “Urusi!”

Katika hafla hiyo, alisema nchi hiyo ilikuwa ikipigania “ardhi zake za kihistoria” nchini Ukraine.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wazimwa kumwandama wakili Danstan Omari

Bei ya stima itapanda mpende msipende, mshauri wa Ruto...

T L