• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
MFALME CHARLES III AVIKWA TAJI: Marais waalikwa wafuatilia hafla kwenye runinga

MFALME CHARLES III AVIKWA TAJI: Marais waalikwa wafuatilia hafla kwenye runinga

NA CHARLES WASONGA

WAGENI wa hadhi ya juu Jumamosi wamehudhuria halfa ya kipekee ya kumtawaza Mfalme mpya Charles III jijini London, Uingereza.

Miongoni mwao walikuwa wafalme, viongozi wa nchi na serikali na hata wasanii mashuhuri.

Viongozi wa ulimwengu waliongozwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, mkewe Rais wa Amerika, Jill Biden, aliyewakilishi mumewe Rais Joe Biden na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Kwa ujumla, miongoni mwa wageni 2,200 waalikwa kwa sherehe hiyo kulikuwa na marais 100.

Kati yao walikuwa ni marais wa nchi ambazo ziliwahi kutawaliwa na Uingereza akiwemo Rais William Ruto wa Kenya.

Pia, walikuwemo marais wa nchi 14 za Jumuiya ya Madola na ambazo ziko chini ya himaya ya Uingereza.

Hata hivyo, wengi wa viongozi na marais waliofika Uingereza kwa sherehe ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III, hawakuruhusiwa kuingia katika ukumbi wa Kanisa la Canterbury ambako sherehe iliandaliwa.

Walilazimika kufuatilia matukio kupitia runinga zilizotundikwa katika kumbi walikoketi.

Hata hivyo, mnamo Ijumaa viongozi hao wa nchi na serikali walijumuika na Mfalme Charles III katika kasri la Buckingham.

Wakati huo huo, Rais Biden ametuma ujumbe wa pongezi kwa Mfalme Charles III na mkewe Malkia Camilla akielezea matumaini kuwa uongozi wao “utadumisha urafiki kati ya Amerika na Uingereza.”

  • Tags

You can share this post!

Rais wa tenisi ya mezani duniani apongeza Kenya kwa kuandaa...

Mbwembwe mfalme akichukua usukani

T L