• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:46 PM
Mfalme Charles III kuongoza nchi 15

Mfalme Charles III kuongoza nchi 15

Na RICHARD MUNGUTI

MFALME Charles III aliyetawazwa jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali atakuwa Rais na Kiongozi wa nchi 15 ulimwenguni.

Mbali na Uingereza na Northern Ireland , Mfalme Charles III atakuwa kiongozi wa nchi 14 kutoka Australia hadi Jamaica zilizokuwa chini ya Himaya ya Harehemu Mama yake, Malkia Elizabeth aliyeaga dunia Septemba 8, 2022.

Kufuatia kifo cha Malkia, Mfalme Charles III alitwaa hatamu za uongozi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Hivyo basi, Mfalme Charles III atakuwa kiongozi wa takriban watu 150 milioni katika Jumuiya ya Madola.

Baadhi ya nchi hizi 15 ni pamoja na Uingereza, Antigua, Barbuda, Belize, Caribbean, Australia, New Zealand, Canada, Bahamas, Grenada, Papua New Guinea, Saint Kitts & Nevis, Saint Lucia, Tuvalu na Solomon Islands.

Wakati wa utawala wa hayati Malkia Elizabeth, nchi 17 zilijitenga na utawala wa moja kwa moja wa Uingereza.

Lakini tangu Mfalme Charles III atwae hatamu za uongozi hakuna nchi kati ya hizo 15 imejiondoa

Alipozuru Antigua na Barbuda 2017, Charles III alisema inapasa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Madola kusalia kuwa na umoja na mwelekeo mmoja.

Katika hotuba yake alisema, “Ni kwa manufaa yetu sote katika Jumuiya ya Madola tujizatiti kujiendeleza na kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.”

Australia iliyojipatia uhuru wake 1901 imekuwa chini ya uongozi wa Malkia Elizabeth.

Malkia Elizabeth alitembelea Australia mara 16 wakati wa utawala wake na watu wa familia yake walitembelea nchi hiyo zaidi ya mara 50.

Charles III alitembelea Australia 1983 akiwa ameandamana na mkewe marehemu Diana.

Charles III hajawahi zuru Bahamas kirasmi ijapokuwa ametembelea nchi hiyo iliyojipatia uhuru wake kutoka kwa Uingereza 1973.

Hali kadhalika, Charles III hajawahi tembelea nchi ya Belize lakini Malkia Elizabeth aliizuru mara mbili, 1985 na 1994.

Charles III ametembelea Canada mara nyingi. Canada ilipata uhuru wake kutoka kwa Uingereza 1867.

  • Tags

You can share this post!

Sheria mpya: Wanaouza pombe haramu kuona cha mtema kuni

Gavana Mung’aro amtetea Pasta Ezekiel akidai wamewahi...

T L