• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Msanii wa Amerika Jason Derulo ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na ngono

Msanii wa Amerika Jason Derulo ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na ngono

NA MERCY KOSKEI

MWIMBAJI wa Amerika Jason Derulo ameshtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na msanii wa kike ambaye alikuwa anarekodi nyimbo kwa kutumia lebo yake.

Kulingana na NBC News, Bi Emaza Gibson mwenye umri wa miaka 25 aliwasilisha malalamishi yake Alhamisi, Oktoba 6, akimshutumu Derulo kwa unyanyasaji wa kijinsia wa ‘quid pro quo’ (fadhili au faida inayotolewa kwa malipo ya jambo fulani).

Gibson alisema alijiunga na lebo hiyo akiwa na matumaini ya kujijengea taaluma.

Alidai kuwa Derulo “Kwa nia mbaya” aliahidi ‘mafanikio’ lakini akamnyima fursa hiyo baadaye.

“Hatua hii ya maisha yangu hivi sasa, inahuzunisha sana. Nina wasiwasi, nina kiwewe. Nimekabiliana na hali za kazi zisizo za kibinadamu,” alielezea NBC News.

Kulingana na hati za korti, Gibson alipewa kandarasi ya kufanya kazi na kampuni ya Derulo ya Future History mnamo Agosti 2021, lakini walianza kufanya kazi pamoja mnamo Novemba mwaka huo huo.

Alidai kuwa msanii huyo hata hivyo, alianza kumtaka kimapenzi na kumshinikiza waende wajivinjari, ombi ambalo aliendelea kulikataa.

Katika kesi iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Kaunti ya Los Angeles, Gibson alidai kuwa Derulo aligeuka baridi baada ya kukataliwa na hatimaye kumfukuza kutoka kwa mpango huo.

Alimshtaki msanii huyo kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono, uvunjaji wa mkataba, vitisho na vurugu, miongoni mwa malalamiko mengine.

Isitoshe, Gibson anadai upotevu wa mapato, fidia iliyoahirishwa, mishahara ambayo haijalipwa na fidia ya dhiki ya kihisia na faida za ajira.

Katika kesi hiyo, aliorodhesha Derulo, meneja wake Frank Harris, RCA Records, Atlantic Records na Derulo’s Future History Imprint zilizo chini ya RCA kama washtakiwa.

Hata hivyo, Derulo, 34, kupitia kwa akaunti yake ya Twitter, alikana madai hayo akisema ni ya uongo.

“Kwa kawaida singetoa maoni, lakini madai hayo ni ya uwongo kabisa na yanaumiza. Ninapinga aina zote za unyanyasaji na ninasalia kumuunga mkono yeyote anayefuata ndoto zake,” alisema.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Rais Ruto, Mwenyekiti wa AU Moussa Faki watofautiania...

Ruto aongoza nchi kumpongeza Kelvin Kiptum kwa kuweka...

T L