• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:15 PM
Rais Ruto, Mwenyekiti wa AU Moussa Faki watofautiania kuhusu vita kati ya Israel na Palestina

Rais Ruto, Mwenyekiti wa AU Moussa Faki watofautiania kuhusu vita kati ya Israel na Palestina

NA LABAAN SHABAAN

KENYA imechukua msimamo tofauti na Umoja wa Afrika (AU) kuhusu vita vinavyoendelea kati ya Israel na Palestina.

Taarifa iliyotolewa na Rais William Ruto inaunga mkono Israel, huku AU ikisema Wapalestina wamenyimwa haki za kimsingi.

“Kenya inaungana na ulimwengu kwa umoja wa Israel na inakashifu ugaidi na mashambulizi kwa wananchi wa taifa hilo wasio na hatia,” Rais alisema kupitia taarifa aliyochapisha katika akaunti yake rasmi ya X (zamani Twitter)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa AU, Bw Moussa Faki amekinzana na Rais Ruto kuhusu ni taifa lipi linafaa kulaumiwa kwa machafuko hayo.

“Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anakumbuka kuwa wananchi wa Palestina walinyimwa haki za kimsingi hasa zile za taifa huru,” ilieleza sehemu ya taarifa ya AU.

Hata hivyo, Rais Ruto na Bw Faki wameungana kwa kauli moja kuhusu kusitishwa kwa mashambulizi pande zote.

Pia, wametoa wito wa kuanzishwa kwa mpango wa maridhiano kuleta amani kati ya Israel na Palestina.

Jeshi la Israel limeripoti kuwa makumi ya watu waliuawa na idadi kubwa kushikwa mateka.

Hii ni baada ya wapiganaji wa Palestina Hamas, kuzindua shambulizi la kushtukiza dhidi ya Israel, Jumamosi Oktoba 7, 2023.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza BBC, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Hamas inawajibika kwa ustawi wao na Israel na “itamchukulia hatua yeyote atakayewadhuru”.

Angalau wapalestina 232 wameuawa na 1, 600 kujeruhiwa baada ya Israel kujibu mashambulizi ya Hamas.

 

  • Tags

You can share this post!

Bei ghali ya maji Nairobi yasababisha wanaume kuparara

Msanii wa Amerika Jason Derulo ashtakiwa kwa unyanyasaji wa...

T L