• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Raia wa kigeni wanaswa msakoni Addis Ababa

Raia wa kigeni wanaswa msakoni Addis Ababa

Na AFP

MAAFISA wa Usalama nchini Ethipia wamekamata mamia ya watu, wakiwemo rais wa kigeni, katika mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa.

Maafisa wa usalama wanalenga watu kutoka kabila la Tigrinya kutoka jimbo la Tigray ambalo limekumbwa na machafuko tangu mwaka jana.Raia wa Amerika na Uingereza ni miongoni mwa watu walionaswa kwenye msako ambao umekuwa ukiendeshwa na maafisa wa usalama tangu kutangazwa kwa hali ya tahadhari nchini humo wiki mbili zilizopita.

Alhamis, serikali imeamuru wamiliki wa nyumba za kupanga wapeleke orodha za wapangaji wao kwa polisi.Serikali ya Ethiopia inasema kwamba inafanya msako dhidi ya watu wanaoshukiwa kuunga mkono waasi wa kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF) ambalo limesema kuwa linakaribia kuteka jiji la Addis Ababa.

Serikali ya Uingereza jana ilisema kuwa imefahamisha serikali ya Ethiopia kuhusiana na kukamatwa kwa raia wake. Kwa mujibu wa ripoti, raia wawili wa Amerika ni miongoni mwa waliokamatwa.

You can share this post!

Mkosoaji wa Kagame atupwa jela miaka 7

Waziri wa masuala ya Kigeni wa Amerika kuanza ziara Afrika

T L