• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:24 PM
Rais Raisi ashambulia nchi zinazolazimisha Uganda kukumbatia mashoga

Rais Raisi ashambulia nchi zinazolazimisha Uganda kukumbatia mashoga

NA MASHIRIKA

KAMPALA, UGANDA

RAIS wa Iran Ebrahim Raisi mnamo Jumatano alilaani mitazamo ya nchi za Magharibi kuhusu ushoga wakati wa ziara yake nchini Uganda.

Aidha Uganda, ndiyo ya kwanza kupitisha baadhi ya sheria kali zaidi za kupinga ushoga duniani.

Raisi akiwa katika dhamira ya kuimarisha uhusiano na safari ya kwanza ya kiongozi wa Iran barani Afrika katika kipindi cha miaka 11, alizikosoa nchi za Magharibi katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Kikao chache na wanahabari kilifanyika baada ya mazungumzo na Museveni.

“Nchi za Magharibi siku hizi zinajaribu kusifia ushoga. Kwa kuendeleza ushoga, wanajaribu kukomesha kizazi cha wanadamu,” Raisi alitangaza.

Museveni alitia saini mswada huo kuwa sheria Mei 29, na kusababisha hasira miongoni mwa mashirika ya kutetea haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na wanaharakati wa LGBTQ pamoja na mataifa yenye nguvu ya Magharibi.

Sheria hiyo mpya inafanya “ushoga uliokithiri” kuwa kosa ambalo mshtakiwa anahukumia kifo na adhabu kwa mahusiano ya watu wa jinsia moja hadi kifungo cha maisha jela.

Raisi aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba nchi za Magharibi “zinafanya kinyume na urithi na utamaduni wa mataifa”.

Kiongozi huyo wa Iran pia alimuunga mkono Museveni kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta na bomba la mafuta ambalo limepingwa na mashirika ya uhifadhi wa mazingira yaliyowasilisha kesi nchini Ufaransa na ukosoaji katika Bunge la Ulaya.

Raisi alisema Tehran iko tayari kubadilishana tajriba yake katika sekta ya mafuta, wakati nchi za Magharibi “hazipendezwi kwa ujumla kuona nchi zinazofurahia rasilimali kubwa na Mbuga za kitaifa kuwa huru”.

Ziara hiyo inajiri wakati Iran inajaribu kupata msaada wa kidiplomasia ili kupunguza kutengwa kwake kimataifa, huku Raisi akitarajiwa kusafiri kwenda Zimbabwe siku ya Alhamisi.

Mnamo Jumatano, alikuwa amekutana na Rais wa Kenya, Dkt William Ruto jijini Nairobi, akielezea ziara yake katika makao makuu ya Afrika Mashariki kama “mabadiliko katika maendeleo ya uhusiano” kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la UBC, baadaye alisafiri hadi Entebbe nchini Uganda, ambako alikaribishwa kwa gwaride la kijeshi na na mbwembwe za mizinga.

  • Tags

You can share this post!

UFAA yashauri Wakenya kufuatilia mali zao zisipotee

Kafyu yatangazwa vijijini kufuatia kero ya Al-Shabaab

T L