• Nairobi
  • Last Updated September 28th, 2023 10:25 PM
Rwanda kuandaa kikao cha marais wa Jumuiya ya Madola

Rwanda kuandaa kikao cha marais wa Jumuiya ya Madola

Na NELSON NATURINDA

KIGALI, RWANDA

RWANDA itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Marais wa Mataifa ya Jumuiya ya Madola (CHOGM) baada ya kikao hicho kuahirishwa mara mbili kutokana na janga la Covid-19.

Mkutano huo utafanyika mnamo Juni 20, 2022.

Tarehe hiyo ilitangazwa Jumanne katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland na Rais wa Rwanda Paul Kagame (pichani).

CHOGM ilipangiwa kufanyika kijiji Kigali June 2020 lakini ikaahirishwa mwaka huo na 2021 baada ya kuamuliwa afya ya wajumbe ingekuwa hatarini wakati ambapo nchini hiyo ilikuwa ikiandikisha ongezeko la maambukizi.

“Rwanda inafurahi kuwaalika wajumbe na washiriki wote jijini Kigali kufanikisha mkutano wa CHOGM. Mkutano huo ni muhimu kwa sababu utajadil changamoto zilizosababishwa na Covid-19 miongoni mwa shida nyingine za kiuchumi,” akasema Bw Kagame.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Ni kinaya Mudavadi kusaliti OKA ilhali...

Usafiri sasa si jinsi ulivyozoeleka Mombasa ‘2/2/22’...

T L