• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Taharuki Farmajo akidai kumfuta kazi Waziri Mkuu Somalia

Taharuki Farmajo akidai kumfuta kazi Waziri Mkuu Somalia

Na MASHIRIKA

MOGADISHU, SOMALIA

TAHARUKI ya kisiasa imezuka nchini Somalia, baada ya Rais Mohamed Farmajo kudai amemsimamisha kazi kwa muda Waziri Mkuu Hussein Roble kutokana na tuhuma za ufisadi.

“Rais aliamua kumsimamisha kazi Roble kwa kuhusika katika ufisadi,” ikaeleza afisi ya Rais kwenye taarifa.Kiongozi huyo alimlaumu Roble kwa kuingilia kesi ambapo anahusishwa na tuhuma za unyakuzi wa ardhi.

Hata hivyo, Roble amekanusha vikali madai hayo, akimlaumu rais kwa “kujaribu kuingilia afisi yake kwa njia ya kijeshi.”

Kando na Roble, rais pia amemlaumu mkuu wa jeshi la maji kwa tuhuma kama hizo.

  • Tags

You can share this post!

Taliban yapiga marufuku wanawake kusafiri bila waume

Visa 103 vya maambukizi mapya ya virusi vya corona...

T L