• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 6:55 AM
Tanzania yakosolewa vikali kufuatia operesheni yake ya kukomesha ukahaba

Tanzania yakosolewa vikali kufuatia operesheni yake ya kukomesha ukahaba

NA MASHIRIKA

DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

SERIKALI ya Tanzania imekosolewa vikali kutokana na vita yake dhidi ya ukahaba kwa kufanya msako katika maeneo mbalimbali Dar es salaam.

Wengi wanaikosoa operesheni hiyo wakisema inaendeshwa kwa njia ya udhalilishaji kwani waathiriwa wananaswa kwenye video na picha yao kuchukuliwa na kuwekwa hadharani.

Baadhi ya nyumba ambazo zinadaiwa kuwa sehemu za madanguro huvamiwa na maafisa wa serikali huku waathiriwa wakimulikwa na kamera na picha zao kuwekwa hadharani.

Ingawa baadhi wanasema hatua ya serikali kukabiliana na ukahaba ni jambo la kusherehekewa, wakosoaji wanasema kuwa kuwamulika waathiriwa hadharani haifai.

Kando na hayo, wakosoaji ambao ni wanaharakati wanasema kuwa kuwaonyesha hadharani waathiriwa ni kukiuka haki yao.

Mwanaharakati, Samsoni Mbunila, anawatupia lawama maafisa wanaendesha operesheni hiyo akisema haijalenga kuleta ufumbuzi wa kudumu katika kukabiliana na tatizo hilo.

Kumekuwa na maoni mengi tangu kutangazwa kuanzishwa kwa opereshini hiyo ambayo haijaelezwa kama itakuwa ya kudumu au la.

Hata hivyo, baadhi ya makundi ya vijana wanadaiwa kuwa karibu na maeneo hayo wamekuwa wakishutumu hatua ya serikali kuyavamia maeneo hayo.

Katika mojawapo ya operesheni zake, mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, aliwaagiza kina dada wote walionaswa kwenye msako huo kwenda kijisalimisha katika vituo vya polisi ili kuhojiwa.

Serikali ilisema uendeshaji wa vikundi vya kikahaba ni kinyume cha sheria ingawa wengi wanaojihusisha na biashara hiyo wanasukumwa na gharama ya juu ya maisha.

  • Tags

You can share this post!

Kindiki afanya mkutano muhimu Lamu kukoleza vita dhidi ya...

Maafisa watatu wa Aimi ma Lukenya kusubiri mwezi mzima...

T L