• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
TZ yatakiwa kuondoa adhabu za kikatili katika sheria zake

TZ yatakiwa kuondoa adhabu za kikatili katika sheria zake

NA BOB KARASHANI

ARUSHA, TANZANIA

MAHAKAMA ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu imeamuru Tanzania kuondoa adhabu za kikatili kutoka kwa sheria zake ili kuzioanisha na Mkataba ulioanzisha mahakama hiyo.

Katika uamuzi wake uliotolewa Ijumaa kuhusu rufaa iliyowekwa na Yassin Rashid Maige dhidi ya kifungo chake kwa miaka 30 kwa kosa la wizi wa mabavu, mahakama hiyo inayoketi Arusha ilisema kuwa mahakama za Tanzania zilikiuka haki za Maige kwa kuagiza acharazwe viboko mara 12 kama sehemu ya adhabu.

Ilisema kuwa adhabu ya viboko iliyoko katika sheria za uhalifu nchini Tanzania inapasa kuondolewa, ili ziafiki kipengele cha 5 cha Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Kibidamu.

Kipengele hicho kinapiga marufuku dhuluma na mateso dhidi ya washukiwa wa uhalifu.Jopo la majaji 11 wa mahakama hiyo limewaamuru maafisa wa Tanzania kuwasilisha ripoti kuhusu jinsi nchi hiyo inavyotekeleza agizo hilo kila baada ya miezi sita “hadi mahakama hii iridhike kuwa utekelezaji huo ni mkamilifu”.

Historia ya Tanzania katika kupinga adhabu za kikatili kwa muda mrefu imejikita katika shule kutokana na visa vya kila mara walimu, na maafisa wa serikali za mashinani, kuitumia kuwaadhibu wanafunzi mbele ya wenzao.

Mfano mmoja ni kisa kimoja kilichotokea mnamo 2021 ambapo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13 katika eneo la Kagera alikufa baada ya kucharazwa na mwalimu wake kwa madai ya kumwibia mwalimu mwingine.

Mnamo Oktoba 2019, Kamishna wa sasa wa Ukanda wa Dar es Salama Albert Chalamila alikemewa vikali na umma alipowatandika wanafunzi 14 wa shule ya upili hadharani kwa madai waliteketeza shule.

Wanafunzi hao walituhumiwa kuanzisha moto uliotekeleza mabweni mawili katika shule yao ya mabweni iliyoko eneo la Mbeya ambako Bw Chalamila alihudumu kama Kamishna wa Eneo.

Ilidaiwa kuwa wanafunzi hao waliteketeza mabweni hayo kulipisha kisasi kutwaliwa kwa simu zao za mkononi na wasimamizi wa shule hiyo.

Licha ya kwamba kitendo cha Chalamila kilishutumia na watatezi wa haki za watoto kote nchini Tanzania, alisifiwa na rais wa wakati huo Hayati John Pombe Magufuli.Katika uamuzi wake kuhusu kesi ya wizi wa kutumia silaha, mahakama ya Afrika haikutofautisha kati ya udhabu ya kikatili katika shule na katika taasisi zingine, kama adhabu kwa vitendo vya uhalifu mkubwa.

Maige amekuwa akitumikia kifungo chake katika gereza la Uyui Central mjini Tabora tangu Septemba 2003 alihukumiwa kwa kosa la wizi alioutekeleza 1999 katika nyumba moja katika Wilaya ya Urambo, eneo la Tabora.

Risasi zilifyatuliwa wakati wa wizi huo, lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Wanahabari wafurushwa Mukumu Girls bweni likiteketea

Upinzani kutumia ujanja mwingine kuikabili serikali

T L