• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Uganda kuanza kuuza mafuta 2025

Uganda kuanza kuuza mafuta 2025

Na DAILY MONITOR

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya mafuta ya Total, Patrick Pouyanne alisema makubaliano matatu ya kuendesha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kati ya Tanzania na Uganda ni hatua kubwa kwa mipango hiyo.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wake, bomba hilo lenye umbali wa kilomita 1,443 maarufu kama EACOP litasafirisha mafuta ghafi kutoka wilaya za Nwoya, Buliisa, Hoima na Kikuube, Uganda hadi Chongoleani, jijini Tanga, karibu na bandari Hindi, Tanzania.

Bomba hilo hasa linalenga kuhakikisha kuwa mafuta ghafi ya Uganda yanauzwa katika masoko ya kimataifa ambapo bei ni juu. Mradi huo unatarajiwa kugharimu Sh407 bilioni ambapo mataifa hayo mawili yatachangisha kila moja pamoja na kampuni za mafuta zinazonuia kuwekeza katika biashara hiyo.

 

You can share this post!

Mwalimu Mkuu alivyojitoa mhanga kufanikisha elimu

Sokomoko mpya Amerika raia mwingine mweusi akiuawa