• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Ukraine yaomba Urusi kukubali mazungumzo

Ukraine yaomba Urusi kukubali mazungumzo

NA MASHIRIKA

KYIV, UKRAINE

UKRAINE imeiomba Urusi kuandaa kikao cha “mazungumzo maalum” kuhusu mkakati wa kuwahamisha wapiganaji na raia waliokwama katika kiwanda kimoja cha kutengeneza chuma jijini Mariupol.

Ombi la Ukraine linafuatia kuibuka kwa video moja iliyoonyesha watu wakiwa wamejificha katika kiwanda cha kutengeneza chuma cha Azovstal, ambapo wanawake kadhaa walisikika wakisema walikuwa wamebakisha tu maji na chakula kitakachowasaidia kwa siku chache zijazo.

Inaaminika kuwa karibu raia 1,000 wa Ukraine wamejificha katika kiwanda hicho, Urusi inapojaribu kutwaa jiji hilo kutoka kwa udhibiti wa majeshi ya Ukraine.

  • Tags

You can share this post!

Mbogo asita kumuunga mkono Sonko Mombasa

Macron ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais

T L