• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Waathiriwa wa mlipuko wazikwa

Waathiriwa wa mlipuko wazikwa

Na MASHIRIKA

MIILI ya zaidi ya watu 100 waliofariki katika mlipuko nchini Sierra Leone wiki jana ilizikwa katika kaburi la pamoja Jumatatu katika eneo la Waterloo.

Majeneza yenye miili hiyo ilisafirishwa kwa malori ya wanajeshi kutoka kwa hifadhi ya maiti katika jiji kuu Freetown hadi eneo la makaburi katika kitongoji cha Waterloo, katika jiji jirani.Malori hayo yalipita katika eneo ambako mlipuko, ambako watu walisimama barabarani kutoa heshima zao za mwisho kwa wahasiriwa hao.

Katika makaburi, jamaa na wafanyakazi, waliovalia mavazi kinga ya kuzika miili hiyo, walifuata malori hayo huku wakiwa wamefunika nyuso zao.Majeneza yalifunikwa kwa bendera ya Sierra Leone yenye maandishi “Rest in Peace” (Lala Kwa Amani).

Yaliwekwa kwenye mstari mmoja wakati wa hafla hiyo ya mazishi iliyoongozwa na Rais wa Sierra Leone Julius Maadio Bio, aliyeandamana na maafisa wengine. “Tutachunguza kilichotendeka,” Bio akasema katika hotuba fupi wakati wa mazishi hayo.

Rais huyo alitoa wito kwa maafisa wa serikali na wanajamii kushirikiana na lengo la kukomesha mikasa kama hiyo kutokea nchini humo wakati mwingine.

You can share this post!

Wakazi wapinga mswada kugawa Kaunti

Wanafunzi 26 wateketea madarasa yaliposhika moto

T L