• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
AFYA: Faida za figili

AFYA: Faida za figili

NA MARGARET MAINA

[email protected]

FIGILI huwa na idadi kubwa ya madini ya sodium, iodine, calcium, magnesium, iron, potassium na phosphorus.

Juisi ya figili pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Juisi ya figili inaboresha mmeng’enyo wa chakula kwa sababu huongeza mzunguko kwenye matumbo. Ni nzuri kwa kuwa husaidia kukabili matatizo ya kufura kwa tumbo na kujaa  gesi, na pia uhifadhi wa maji mwilini.

Pia husaidia kudhibiti asidi ya tumbo.

Juisi ya figili hupunguza lehemu mbaya katika mfumo wetu wa damu. Utafiti unaonyesha kuwa figili husaidia kupunguza shinikizo la damu kwa kufanya kazi kama kipumzisha-misuli, kuboresha mtiririko wa calcium na potassium kwenye seli na kuruhusu mishipa ya damu kupanuka na kusinyaa kwa urahisi zaidi.

Sodium kwenye figili husaidia kuleta utulivu wa shinikizo la damu.

Husaidia ini. Figili husaidia kupunguza mkusanyiko wa mafuta kwenye ini. Virutubisho vilivyomo kwenye figili hulinda ini na kutoa vimeng’enya vinavyosaidia kusafisha mafuta na sumu.

Juisi ya figili huponya utumbo ikitusaidia kusaga vitu kwa haraka na kwa ufanisi zaidi na kuzuia asidi kuongezeka na vidonda.

Figili imejaa vitamini na madini muhimu kama vile potassium, folate, vitamini K, vitamini B6 na vitamini C na ni nzuri kwa ngozi.

Njia bora ya kunywa juisi hii ni kuinywa asubuhi kwenye tumbo tupu, peke yake.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Vidakuzi vya siagi ya karanga

Kiunjuri, Mbunge waagizwa kufika mbele ya IEBC

T L