• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:42 PM
Atumia teknolojia ya 3D kutengeneza vipuri ambavyo vinginevyo vingeagizwa kutoka nje

Atumia teknolojia ya 3D kutengeneza vipuri ambavyo vinginevyo vingeagizwa kutoka nje

NA MAGDALENE WANJA

KUTAFUTA suluhu ya changamoto ni mojawapo ya njia zinazochangia katika ubunifu mkubwa duniani.

Kuleta suluhu imekuwa ndoto kuu ya Mehul Shah ambaye ni mhandisi wa mitambo.

Alipokamilisha masomo yake nchini Uingereza, alirejea humu nchini na kufanya kazi katika viwanda vya nguo (textiles), ambako aligundua kuwa kulikuwa na changamoto ya kupata vipuri kila mashine hii au ile ilipata hitilafu.

“Changamoto hizo zilifanya nifikirie sana kwani tatizo kubwa ni kwamba vipuri hivi havikupatikana humu nchini, na ilibidi kuagiza kutoka nchi za nje,” akasema Shah.

Kando na kuchukua kuda mrefu kuwasili nchini, vilikuwa nna bei ya ghali sana.

Mehul Shah ambaye ni mhandisi wa mitambo akiwa kiwandani anamoendeshea shughuli zake za utafiti, ubunaji na utengenezaji wa bidhaa na vipuri. PICHA | MAGDALENE WANJA

Njia mbadala ilikuwa kuagiza kutoka kwa sekta ya juakali ambayo ilichukua muda kuunda vipuri hivyo.

“Mnamo mwaka 2014, kwa ushirikiano na rafiki yangu tulianziasha kampuni ambayo ingeweza kupunguza mzigo huo kwa kutengeza vipuri nchini kwa kutumia teknolojia ya 3D,” anaongeza.

Punde tu walipoanza biashara hio, kampuni nyingi ambazo zilitaka miundo mbalimbali ya bidhaa za plastiki zilijitokeza na kutaka kushirikiana.

“Tulianza kwa kujifunza aina mbalimbali za miundo,” aliongeza.

Teknolojia imesaidia katika kuunda sampuli za bidhaa kwa baadhi ya kampuni humu nchini.

Mehul Shah ambaye ni mhandisi wa mitambo akiwa kiwandani anamoendeshea shughuli zake za utafiti, ubunaji na utengenezaji wa bidhaa na vipuri. PICHA | MAGDALENE WANJA

Hii ni pamoja na kuunda vipuri, vifaa katika sekta ya afya , magari au mikebe ya kupaki bidhaa mbali mbali.

Shah anaongeza kuwa mambo yalibadilika sana wakati wa janga la Covid na vita katika nchi ya Ukraine, jambo ambalo lilifanya kuagiza vipuri kuwa vigumu zaidi.

Kampuni hiyo imepata wateja wengi ambao wamechangia katika ubunifu zaidi na kupunguza mzigo wa kuagiza.

“Katika kampuni ya Ultra Red Technologies, tunaunda bidhaa katika dizaini za 3D ambazo hutumika kama sampuli za kuunda bidhaa zaidi,” anaongeza.

Ndoto yake kuu ni kutoa huduma katika nchi nyingine ili kuleta suluhu ya haraka na kwa bei inayoshikika.

Mehul Shah ambaye ni mhandisi wa mitambo akiwa kiwandani anamoendeshea shughuli zake za utafiti, ubunaji na utengenezaji wa bidhaa na vipuri. PICHA | MAGDALENE WANJA
  • Tags

You can share this post!

Azimio yapeleka ajenda kwa MCAs

Kalonzo hasaidiki, adai Rais

T L