• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Bajeti 2023/24: Idara ya Polisi yatengewa Sh800 milioni kuboresha magari

Bajeti 2023/24: Idara ya Polisi yatengewa Sh800 milioni kuboresha magari

NA SAMMY WAWERU

IDARA ya Kitaifa ya Huduma za Polisi (NPS) imepata mgao wa Sh800 kusaidia kuboresha magari.

Waziri wa Fedha na Hazina ya Kitaifa, Prof Njuguna Ndung’u alisema Alhamisi, Juni 15, 2023 wakati akisoma Makadirio ya Bajeti 2023/24, mgao huo utasaidia idara ya polisi kuimarisha huduma za usalama kwa umma.

“Hali kadhalika, Idara ya Polisi itapata mgao wa Sh850 milioni kuboresha maabara ya uchunguzi na utafiti wa kiusalama,” Prof Ndung’u alielezea.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, kabla kustaafu 2022 alizindua maabara ya kisasa katika makao makuu Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI).

Kwa muda mrefu, maafisa wa polisi wamekuwa wakilalamikia upungufu wa magari kuendeleza huduma za usalama kiasi cha kushinikiza umma kutoa pesa kugharamia mafuta.

  • Tags

You can share this post!

Bajeti 2023/24: Serikali kuondoa ushuru wa unaotozwa gesi...

Bajeti 2023/24: Waziri Ndung’u asema ni heri sukari...

T L