• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:55 PM
Asingekuwa na mwito, mwenge wa uimbaji ungezima

Asingekuwa na mwito, mwenge wa uimbaji ungezima

Na PATRICK KILAVUKA

Ulaghai wa nyimbo zake ungemshusha moyo kama mwandamu! Lakini aliamini kwamba Mwenyezi Mungu aliyempa hekima na neema ya kipaji atamfungilia milango ya kueneza injili.

Isitoshe, mwenge wa kuchochea uimbaji na maono utadhihirika. Kuna watu ambao wanajihitaji tu upendo na kuwajali ili, wapate kuweka matumaini yao kuwa hai. Japo wanajihisi kutengwa ni wanadamu kama wengine! Kuwahimiza

kwa sababu Maulana anawajalia. Hamna aliye uwezo kuliko mwingine kwani wote ni kazi ya Mola na utu ndio ubinadamu!

Hii ni kauli ya msanii na mhubiri Agnes Njeri Muturi ambaye anahudumu na huduma ya Pick Propheting Ministry, Kayole. Anasema kuna msichana mmoja aliyepata neema ya uponyaji alipokuwa ametembelea nchi ya Uganda kupitia huduma yake baada ya kumtendea wema na kumuonyesha upendo ingawa alikuwa ametendewa uovu na kuacha na machungu ya moyo.

Agnes Njeri Muturi wakati wa alipokuwa akirekodi kwenye studio .Picha /Patrick Kilavuka

Ila, alipomjalia na kuonyesha upendo, alianza kuwa na matumaini ya maisha na akapona.

Msanii/ mhubiri Njeri alizaliwa Githima kaunti ndogo ya Kigumo, Kaunti ya Muranga.

Alisomea Shule ya Msingi ya Githima kabla kujiunga na Sekondari ya Shule iyo hiyo na kwa sababu ambazo hangeziepuka alifika kidato cha pili. Ameolewa na kubarikiwa watoto wanne; wavulana watatu na binti mmoja.

Alianza kuangazia usanii wake akiwa shule ya msingi kwani alikuwa mwandishi mzuri wa mitungo na mashairi. Fauka na kuwa sauti ya ninga.

Akiwa darasa la nne, mizizi ya uimbaji ilikuwa imeota na alikuwa anapenda sasa kusikiza nyimbo kwenye redio ya KBC pindi tu babaye alipokuwa ameifungua.

“Nyimbo hizo zilinipa uhondo na utamanifu wa kufinyanga kipaji cha uimbaji. Nilipofika darasa la nane, nilikuwa nimeiva kiusanii kwani kupitia weledi wa utunzi mashairi, niliuoanisha na uimbaji wangu na kuanza kuwa na mawazo pevu ya kutunga nyimbo,” akafichua msanii Agnes ambaye amerekodi nyimbo kadhaa na video.

Nyimbo zake zinalenga maudhui ya matukio ya kiunabii, hali za maisha, kuabudu na kusifu Mola. Ufunuo mwingine unatokana na kulisoma Neno, kuomba na kufunga ambapo hupata jumbe ambazo hutumia kupalilia kipawa chake.

Nyimbo ambazo amezinasa, anaziangazia kwenye Youtube Aggy-Angelique ni Thiini Iracinwo( Dunia itachomwa), Ndiri na thiina na mirii( msitazamia nambolea ya mwili), Nakuabudu, Ukai Mwone na Itumi ngiri na ngiri (sababu elfu za kusifu).

Zile ambazo ziko kwenye video ni Ukai mwone( muone matendo), itumi ngiri na ngiri( sababu elfu za kusifu, Ndikwa (sitakufa) , Turekere(tusamahe), Nionjeshe utamu wako, We Ngai na Uthaa ria Grace.

Anasema huduma yake ilianza kama angali mchanga kwani akiwa ndogo, alikuwa anaona maono na pasi na kujua ubayana wa kiroho. Japo alianza kuelewa wakati alipoanza kufafanuliwa huku akijengwa kimiani.

Yeye ameamini kwamba kunao masalio ya watumishi wa kweli kulingana na Biblia na ni vyema kuwatambua. Picha/ Patrick Kilavuka

 

Anasema muziki wa moja kwa moja ulikuwa bora na njia ya kupasha ujumbe kwa wengi ingawa corona sasa imeyumbisha mtagagusano wa watu.

Hata hivyo, anasema kila tukio lina makusudi yake kwani katika kila hali Mungu hujidhihirisha.

“Majanga ndiyo Mungu alikuwa anatumia watu wanapomuasi ili wamrudie,” asema mtumishi/ mwimbaji huyo.

Changamoto ambayo amekubana nayo katika usanii ni ughushi wa nyimbo. Kihuduma ni kwamba, watu hawaamini huduma ya unabii ilivyokuwa enzi za kale za manabii, japo kuna masalio wa ukweli ambao wanaweza kutwezwa lakini Maulana akatenda makusudio yake.

Ushauri wake ni kwamba waimbaji watumie majukwaa ya kuenezi injili kusawazisha maisha ya wanadamu, waimbe na kutunga nyimbo za ukubwa wa Neno kwa sababu uimbaji si wa kutumbuiza tu bali ni utumishi unaofanywa.

You can share this post!

Alaba afunga bao na kusaidia Real Madrid kunyanyasa...

Aibu wahuni wakiteka siasa

T L