• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Baada ya kugawanya mashabiki kwa ‘Nataka Kunyonywa’, Embarambamba aibuka na ‘Panua’

Baada ya kugawanya mashabiki kwa ‘Nataka Kunyonywa’, Embarambamba aibuka na ‘Panua’

NA WANDERI KAMAU

MWANAMUZIKI tatanishi wa nyimbo za injili ‘Embarambamba’ kutoka eneo la Gusii, sasa amerejea na kibao kipya kiitwacho ‘Panua’, siku chache baada ya kuwatumbuiza mashabiki wake kwa kibao ‘Nataka Kunyonywa’. 

Mwanamuziki huyo, kwa jina, Christopher Nyangwara Mosioma, alitoa kibao hicho mnamo Jumapili, mistari yake ikizua migawanyiko mikubwa miongoni mwa mashabiki wake.

Unaeleza wimbo huo: “Panua Yesu, panua wagonjwa wapone…panua maisha yetu…”

Kabla ya nyimbo hizo mbili, alikuwa pia ametoa kibao ‘Nimwagie’, ambacho pia alidai ni cha injili, na lengo lake kuu ni kumtukuza Mungu.

Hata hivyo, majina anayozipa nyimbo zake yamezua gumzo miongoni mwa Wakenya, baadhi wakisema anawapotosha mashabiki wake.

Wengine walisema semi zake zinarejelea masuala ya uasherati, hivyo kukinzana na injili ya kweli.

“Bila shaka, semi za nyimbo hizo zinarejelea masuala ya uasherati. Anawianisha utunzi wake na masuala ya injili, ila kuna jumbe fiche za kiuasherati,” akasema Bi Eva Mong’ina kupitia mtandao wa YouTube.

Licha ya ukosoaji ambao amekuwa akipokea kutoka kwa mashabiki wake kutokana na majina anayozipa nyimbo zake, mwanamuziki huyo alisema atafanya kila awezalo kuhakikisha amezua gumzo miongoni mwa mashabiki.

Kando na semi hizo, pia huwa anatumia mitindo tata ya uimbaji, kama vile kupanda miti, nyumba au hata kuwafukuza watu na wanyama.

“Niko tayari kufanya lolote ili kuwateka mashabiki wangu. Hivyo, huwa sijali yanayosemwa kunihusu,” akasema mwanamuziki huyo.

  • Tags

You can share this post!

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale awasilisha ombi akitaka...

Lamu yadai ndicho kitovu cha ukale ikitaka iwe mwenyeji wa...

T L