• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
Brian Chira aweka kiburi kando, aomba msamaha kwa waliomsaidia

Brian Chira aweka kiburi kando, aomba msamaha kwa waliomsaidia

NA FRIDAH OKACHI

MTENGENEZAJI maudhui kwenye jukwaa la TikTok, Brian Chira, ameomba msamaha kwa mara nyingine kufuatia matamshi yake machafu mtandaoni, yaliyolenga waliomsaidia. 

Kijana Brian anadai kuwa kwa muda wa siku tatu mfululizo zilizopita, amekuwa akitatizika kutokana na ugumu wa maisha.

Awali, baadhi ya wafuasi wake walijitokeza kumsaidia kwa hali na mali.

Aidha, alichangiwa zaidi ya kima cha Sh400,000.

“Baba Talisha na Nyako, mmenifanyia mambo makuu. Naomba mnisamehe,” akasema Brian kupitia video aliyopeperusha moja kwa moja mnamo Jumatano, Septemba 27, 2023.

Ombi la msamaha linatokana na mahojiano aliyofanya na Presenter Ali yaliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo alikana kupokea msaada kifedha.

Brian alidai kuwa Bi Nyako hakumsaidia kwa chochote kile.

Kutokana na ulimi wake mchafu, Nyako ambaye pia ni Mwanatiktoker, alitishia kumchukulia hatua kali kisheria.

Mwigizaji huyo alilalamkia kuchafuliwa jina.

Pilot Niako kama anavyojitambua Tiktok, almaarufu Nyako, ni Mkenya anayeishi Ujerumani na familia yake.

Nyako alitumia ushawishi wake mitandaoni kuleta mashabiki pamoja wakachangia Brian Chira  kima cha Sh430,000, pesa ambazo zilitumika kusaidia barobaro huyo, ikiwemo kumlipia kodi ya nyumba hadi mwaka ujao, 2024.

Kando na Bi Nyako, kupitia Tiktok, Baba Talisha alisema kuwa baada ya mchango huo wa pesa, walihakikisha kuwa kodi ya nyumba  anakoishi Brian Chira imelipwa.

Nyako, amekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa msanii huyo tata hajipati kukwaruzana na sheria.

Hii ni baada ya kuzungumza naye Azziad Nasenya akimuomba kutupilia mbali kesi aliyokuwa amemshtaki Agosti 2023.

Brian anasemekana alimrushia Azziad cheche za matusi kwenye Tiktok Live.

Bi Nyako alimsihi Azziad kutupilia mbali kesi hiyo, akisisitiza kuwa Brian Chira anaugua na anahitaji usaidizi wa kimsingi kutoka kwa waigizaji.

Alikuwa ameshtakiwa katika mahakama ya Kibra.

Kabla kufikishwa kortini, alikuwa amekesha siku kadha katika kituo cha polisi.

  • Tags

You can share this post!

Kauli za Ndii zaashiria kuna nyufa katika Ikulu ya Rais?

Idara ya afya kaunti ya Nairobi yamulikwa kwa kutoa vyeti...

T L