• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Diamond Platnumz amsifu Raila akisema mwanasiasa huyo ndiye ‘Baba Lao’

Diamond Platnumz amsifu Raila akisema mwanasiasa huyo ndiye ‘Baba Lao’

NA WINNIE ONYANDO

MSANII maarufu wa Bongo Flava, Diamond Platnumz, katika mahojiano ya kipekee na Taifa Leo amefichua kuwa bado ana ukuruba na kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya, Raila Odinga.

Diamond alikiri hayo Jumamosi katika hoteli ya Serena kabla ya Tamasha la Tusker Oktobafest huko Ngong Racecourse.

Gari ambalo Diamond Platnumz ametumia kufika katika hoteli ya Serena. PICHA | WINNIE ONYANDO

Ikumbukwe mwanamuziki huyo mashuhuri alipiga shoo kali katika hafla ya kisiasa ya Azimio iliyofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Kasarani mnamo Agosti 6, 2022, ambapo alilipwa takriban Sh1.2 milioni.

Alipoulizwa ikiwa amezungumza na Bw Odinga baada ya kupoteza katika uchaguzi wa urais mwaka wa 2022, Diamond alijibu kwa kusema, “Ndiyo, tushawahi kuzungumza. Nilikuja, nikapiga shoo na kila kitu kilikuwa sawa.”

Hiyo ndiyo ilikuwa shoo fupi sana kuwahi kufanywa na mwanamuziki huyo.

Akiwa Kasarani, Diamond Platnumz alifanya shoo kwa awamu mbili, moja moja kabla ya Bw Odinga kuzungumza na nyingine baada ya Bw Odinga kuhutubu.

Alianza kwa kutoa wimbo wake wa 2019, ‘Baba Lao’, akiubadilisha ili kumsifu Raila Odinga na mgombea mwenza wake, Bi Martha Karua.

Diamond alirudi jukwaani mwishoni mwa hotuba ya Bw Odinga, ambapo alijiunga na viongozi wengine wa Azimio na Mama Ida Odinga. Aliingia tena jukwaani na baadaye akaondoka kwa helikopta kuelekea nchini Afrika Kusini.

Kwa upande mwingine, Diamond alisema kuwa ana mpango wa kufanya kolabo na mwanamuziki wa humu nchini. Hata hivyo, hakumtaja mwanamuziki huyo.

Kando na hayo, alisifu Kenya akisema kuwa anajihisi kuwa yuko nyumbani.

“Kwanza napenda Kenya. Ikumbukwe kuwa mwanangu ana mzazi kutoka hapa Kenya. Mamake ni Mkenya, Hivyo, najihisi niko nyumbani,” akasema.

Diamond aliwasili nchini Ijumaa na anatarajiwa kupiga shoo kali huko Ngong Racecourse leo Jumamosi.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume azama baharini baada ya kuokoa mwanamke na mtoto

Watu sita wafunikwa na udongo wa maporomoko ya ardhi Kisauni

T L