• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Ex wa Diamond Hamisa Mobetto kufanya kazi na hasimu wa Wasafi, Konde Boy

Ex wa Diamond Hamisa Mobetto kufanya kazi na hasimu wa Wasafi, Konde Boy

NA FRIDAH OKACHI

MWIGIZAJI Hamisa Mobetto amesema anarudi kwenye muziki, akitarajiwa kushirikiana na mwanamuziki Harmonize.

Akizungumza kwenye sherehe za Samaki Samaki nchini Tanzania, mwigizaji huyo amesema mazungumzo yanaendelea.

Hamisa ambaye pia ni mfanyabiashara, alisema kuchukua pumziko la muda ni uamuzi uliotolewa na usimamizi wake.

“Kufanya muziki ni hobby kwangu. Usimamizi ndio uliamua nichukue mapumziko ya muda. Kuhusu kufanya muziki na Harmonize, mazungumzo baina yake na usimamizi wangu yanaendelea. Ila sijui yamefikia wapi,” alisema Hamisa.

Akihojiwa na Rick Media, mwigizaji huyo alionekana kushikilia msimamo wake wa mahusiano na mpenzi wake wa sasa anayefahamika kama Kelvin.

“Mimi ndiye niliyewaleta kwenye ulimwengu wangu wa mapenzi. Mahari yamelipwa lakini wakati ukifika wa kuhalilisha ndoa yangu nitawafahamisha,” alisema Hamisa.

Juma lililopita, Harmonize alimwalika Hamisa kwenye maandalizi ya hafla moja ambayo matokeo yake hayakufikia malengo.

Kwenye shamrashamra hizo, palikuwepo na video moja ikionyesha mwanamuziki Harmonize akiwa amevalia vazi lilikokuwa limechapishwa picha ya mfanyabiashara huyo.

Video hiyo Harmonize alisikika akimwambia aliyekuwa akimrekodi aondoke baada ya kusema kuwa Harmonize anadhihirisha mapenzi kwa mwanadada huyo.

“Chukua hela uondoke,” alisema Harmonize.

Wakati wa maandalizi ya hafla hiyo, Harmonize alihojiwa na kituo cha Cloud Media kuhusiana na uhusiano wao.

Alisema wakati fulani wote walikuwa marafiki wakiwa kwenye mahusiano tofauti na walipitia wakati mgumu.

“Wakati huo alikuwa kwenye uhusiano hadi wakatapa mtoto. Hakuna jinsi ningesema nampenda, ingekuwa ni kama nalipiza kisasi,” alisema Harmonize.

“2013 nilipitia vikwazo vingi, lakini haimanishi naweza kaa miezi sita bila kujipata kwenye mahusiano mengine. Kipindi hicho nilipitia vipindi vigumu kwa kujitafutia. Kila msichana niliyekuwa naye alitumia pesa ambazo ningekuwa nampa mwanamke mmoja wa Kitanzania,” aliongezea Harmonize.

  • Tags

You can share this post!

Mama, 75, ashinda kesi ya kufurusha wanawe wa kiume...

Mshairi anayeishi na ulemavu wa ngozi ajizolea sifa ndani...

T L