• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
Hivi mnajua anachofanya mkewe Guardian Angel kudumisha shepu mnayoiona?

Hivi mnajua anachofanya mkewe Guardian Angel kudumisha shepu mnayoiona?

NA SINDA MATIKO

MKE wa msanii wa injili Guardian Angel, Esther Musila mwenye umri wa miaka 52, amefichua siri ya umbo na mwonekano wake wa ujana.

Licha ya kuwa kamzidi mume wake na miaka 18, Musila amekuwa akiwakosha wengi na shepu yake ya nyungu.

“Nafanya mazoezi sana na mazoezi yangu ni kudensi napenda sana. Kuhusu shepu, nafikiri ni maumbile. Wajua nilikuwa mwembamba sana kwenye miaka yangu ya 30 na 40 ila ghafla niliongeza uzito kipindi cha Covid-19. Lakini wajua mwanamke anapotimiza miaka 50, huwa anaongeza uzito kwa haraka sana kutokana na mabadiliko ya homoni.”

Kando na mazoezi Musila anasema huwa makini sana na suala la lishe.

“Huwa sili chakula kingi cha kwanza hicho. Pili naepukana sana na vyakula vya ngano na pia sukari mimi sio mtumizi.Halafu nanywa maji sana pamoja na kula mboga kwa wingi. Kwa siku huwa ninakula mara mbili tu usiku nanywa chai tu tena bila sukari,” Musila anasema.

***

DJ Pierra: Natamani mtoto lakini…

DJ Pierra Makena. PICHA | POOL

DJ PIERRA Makena anasema licha ya kuwa umri wake umesonga, na kama sio hekaheka zake za kutafuta hela, basi angewazia kupata mtoto wa pili.

Mrembo huyo mwenye miaka 42, ana binti mmoja tu mwenye miaka saba.

Pierra anasema alimpata katika mazingira magumu sana na ndio sababu wazo la kupata wa pili, halimwingii kichwani.

“Mwanzo unafahamu mimi ni mtumbuizaji hivyo kila kukicha nipo mbioni kwenye pilkapilka za hapa na pale kusaka mpunga.
Nimemlea binti yangu kwenye mazingira ya mara nyingi unakuta sipo, kwa sababu lazima nimtafutie. Unakuta mara nyingi wakati nipo nahitaji kulala ili niweze kuamka nikatafute. Ila inanilazimu sasa niusulubishe usingizi wangu ili kuwa na binti yangu. Halafu eti uniambie niongeze mtoto mwingine, ” anasema.

Aidha Pierra anasema kwenye malezi ni yeye tu ndiye mzazi kwani mzazi mwenzake alishawatoka zamani.
  • Tags

You can share this post!

Kenya kulipwa mabilioni ili kusafisha uchafu wa Saudi Arabia

Mawaidha ya Kiislamu: Tuthibitishe tunamhusudu Mungu...

T L