• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Kidume cha mbegu: ‘Manzi wa Kibera’ na mumewe wa miaka 67 watarajia mtoto wa kwanza

Kidume cha mbegu: ‘Manzi wa Kibera’ na mumewe wa miaka 67 watarajia mtoto wa kwanza

NA MERCY KOSKEI

SOSHOLAITI kwa jina Sheriffa Wambui, almaarufu Manzi wa Kibera na mumewe wa miaka 67 Samuel Nzuki Ndunda kwa jina la utani Fundi Kijana wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Manzi wa Kibera aliwajuza wafuasi wake habari hizo za furaha kwa kuchapisha picha akiwa ameshika tumbo lake huku akiitazama kwa fahari.

Katika chapisho hilo la Oktoba 25,2023, Manzi wa Kibera aliendelea kwa kusema kuwa wana furaha na baraka tele baada ya kupokea habari hizo.

“Wakiwachana na sisi ndio tunapendana,” alisema.

Manzi wa Kibera alichapisha video, akiwa na mpenziwe huyo wakiwa studio wakirekodi kitu huku akicheza na kuwachokoza mashabiki kuwa labda wanatayarisha wimbo pamoja.

Wawili hao wamekuwa wakichumbiana tangu 2021.

Hata hivyo, mashabiki walibaki na maswali mengi huku wengine wakisema ni mbinu ya kutafuta wafuasi mtandaoni (cloutchasing).

Hata hivyo, wawili hao walikanusha tetesi hizo wakisisitiza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Wengi walifurika kwenye safu ya maoni, kutoa hisia zao tofauti.

Jimal  roho safi  alisema,”Kwani it was that serious”?

Vibing rizzy “mtoto atazaliwa na kihara”.

  • Tags

You can share this post!

DPP kutathmini upya kesi ya wizi wa Sh122 milioni dhidi ya...

Mwanamume ashtakiwa kujifanya wakili na kumwakilisha Sheng...

T L