• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Mwanaharakati Boniface Mwangi akaangwa mitandaoni baada ya kuhukumiwa kifungo jela kwa kuikaidi mahakama

Mwanaharakati Boniface Mwangi akaangwa mitandaoni baada ya kuhukumiwa kifungo jela kwa kuikaidi mahakama

NA FRIDAH OKACHI

MWANAHARAKATI Boniface Mwangi amehukumiwa atumikie kifungo cha miezi miwili endapo atashindwa kulipa faini ya Sh300,000 kwa kukiuka mahakama.

Jaji Francis Rayola wa Mahakama Kuu ya Machakos ametoa hukumu hiyo kwenye kesi iliyowasilishwa na Waziri wa Utalii na Wanyamapori Alfred Mutua akidai mwanaharakati huyo alimchafulia jina.

“Nimepatikana na kosa la kudharau Mahakama. Nitafungwa miezi miwili au nilipe faini ya Sh300,000. Agizo lilitolewa hadi Januari 2024. Siwezi tena kuchapisha ni nani alilipua nyumba yangu kwa bomu. Kila mtu anajua aliyelipua nyumba yangu,” alichapisha Bw Mwangi kwenye ukurasa wa Facebook.

Baadhi ya mashabiki wakiweka maoni kwenye chapisho hilo, wamemkaanga kwa kudharau mahakama.

Fasbolt Kadenge amesema: “Fuata Sheria namna wewe hutaka Sheria ifuatwe.”

Naye Sammy Kimani amesema ni wazi hatakuwa jela.

“Nakushauri uwe na busara kwenye machapisho yako. Usiwe mgomvi sana hata pale ambapo hakuna maana,” akasema Kimani.

Akaongeza: “Wewe ni mzuri lakini acha marafiki wako wakuu wakushauri kila wakati, sababu una utata. Furahia chakula cha jioni.”

Naye Kamau Wa Mbari amesema: “Ulidharau mahakama, hauko juu ya sheria.”

Kwenye uamuzi huo ambao ulitolewa na Mahakama Kuu ya Machakos, mwanaharakati huyo aliwakilishwa na Wakili Mkuu (SC) Bi Martha Karua.

Kumpa sapoti wamekuwepo wandani wake Mwanaharakati na Mkurungezi mkuu wa Shirika la Haki Africa Bw Hussen Khalid na mwanamuziki Julias Owino almaarufu Juliani miongoni mwa wengine.

Oktoba 2023, mwanaharakati huyo alidai ubomoaji wa ardhi ya Mavoko unasababishwa na viongozi na watu walaghai.

Katika chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Mwangi alisema waliofukuzwa kwenye ardhi hiyo ni watu wanaoimiliki kihalali.

  • Tags

You can share this post!

Mimi ni tasa, miaka 2 sijaambia mume wangu. Nishauri

Kamati ya Mazungumzo yarejelea mapumziko kunakili mbinu za...

T L