• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Size 8: ‘Vidonge’ ni kibao kilichonitoa matopeni

Size 8: ‘Vidonge’ ni kibao kilichonitoa matopeni

NA SINDA MATIKO

KILA mtu ana stori yake ya ufanisi na yake mwimbaji mhubiri Size 8, ilitokana na hiti ya ‘Vidonge‘.

Size 8 Reborn kafichua kuwa baada ya kushindwa kujiunga na Chuo Kikuu kutokana na umaskini, aliamua kusaka hela.

Siku moja alisikia kuna usaili wa shindano la uimbaji la Tusker Project Fame alikokwenda kujaribu bahati yake ila hakutoboa.

Lakini kwenye heka heka hizo, alikutana na produsa mkongwe Clemmo, mwasisi wa mojawapo ya lebo kubwa za muziki kuwahi kutokea Calif Records.

Clemmo aliishia kumsaini Size 8 kwenye lebo hiyo ya Calif.

Ingawaje hakuwa na hela, Clemmo alimsaidia Size 8 kurekodi hiti yake ya kwanza ‘Shamba Boy’.

“Bado nilikuwa naisha kimaskini sana nilipotoa ‘Shamba Boy’. Lakini baada ya wimbo huo kuchezwa sana Kiss FM ambayo ilikuwa ndiyo stesheni ya redio iliyokuwa ikivuma miaka hiyo, ndipo niliweza kupata shoo zangu za kwanza,” Size 8 anasema.

Ingawaje shoo hizo hazikuwa zikilipa vizuri sana, Size 8 anasema aliweza kujiwekea akiba ya kiasi cha Sh230,000 hela ambazo anasema alizitumia zote kwenye ngoma yake iliyofuata na ikaishia kuwa ngoma iliyombadilishia maisha kabisa.

“Ilifika wakati nikahisi nilihitaji kuipelekea brandi yangu katika levo nyingine. Nikaamua kucheza kamari ya pata potea. Nilinunua ndengu za kutosha na makaa, na nikalipa kodi ya nyumba kwa miezi mitatu ili zije kunishikilia mambo yakienda mrama. Fedha zilizosalia zote nikawekeza kwenye kurekodi ngoma na Ogopa DJs. Enzi hizo ukirekodi ngoma na Ogopa DJs basi wewe ni staa,” akaeleza.

Baada ya kurekodi ‘Vidonge’ chini ya Ogopa, Size 8 anasema mchezo wake wa bahati nasibu ulilipa.

“Vidonge ilinibadiishia maisha. Ngoma hiyo ilipotoka, miezi miwili baadaye nilianza kupata shoo kubwa kubwa zilizonilipa kiasi cha pesa ambazo sikuwa nimeona. ‘Vidonge‘ ndio ngoma iliyonibadilishia maisha,” anakiri Size 8.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Nina furaha wanawake wengi Mlima Kenya wana mimba...

Kioni: Ruto anataka kubadilisha Katiba kupitia mlango wa...

T L