• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Bloga wa Jubilee Pauline Njoroge adai kuibiwa Sh300, 000 alipokamatwa na DCI

Bloga wa Jubilee Pauline Njoroge adai kuibiwa Sh300, 000 alipokamatwa na DCI

NA SAMMY WAWERU

MWANABLOGU wa chama cha Jubilee, Pauline Njoroge amedai kwamba aliibiwa kima cha Sh300, 000 alipokamatwa na makachero wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu na Jinai (DCI) Julai 2023, Malindi, katika Kaunti ya Kilifi.

Kupitia chapisho la Facebook, mnamo Jumanne, Agosti 15, Bi Pauline aliambia wafuasi wake kwamba pesa hizo zilitolewa kwa njia ya kimitandao – kidijitali.

Pamoja na mwandani wake, Jane Mwangi Nduta na dereva wa teksi walimokuwa, Emanze Jilani, alikamatwa kwa tuhuma za kuwa na dawa za kulevya na kuchochea upinzani dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.

Watatu hao walitiwa nguvuni katika barabara ya Watamu-Jakaranda, na kuzuiliwa siku kadha kwenye Kituo cha Polisi cha Watamu.

“Jioni ya Agosti 3, 2023, kima cha Ksh 302, 842 kilitolewa kutoka kwenye akaunti yangu kwa ujuzi wa kimitandao,” Pauline aliandika katika akaunti yake ya Twitter na ukurasa wa Facebook.

Bloga huyo anayezidi kukosoa utawala wa Dkt Ruto, alifichua kwamba suala hilo lilikuwa miongoni mwa mambo yaliyowekwa paruwanja na kikosi cha mawakili wake katika kesi iliyosikizwa mnamo Jumatatu, Agosti 14.

Wakili Ndegwa Njiru ni mmoja wa mawakili wa Pauline.

“Maafisa wa DCI ndio pekee ‘walimiliki’ kadi zangu za benki kabla ya wizi huo.”

Katika masimulizi, alipakia chapisho la mtumizi wa Facebook aliyeamini alikuwa anaelewa utapeli ulivyosakatwa.

“Asubuhi ya Agosti 4, 2023 akaunti ya Facebook yenye utambuzi – Mary Mukami (ingawa ni bandia), mtumizi alijua walichofanya,” alidokeza.

Bloga huyo ambaye ni mwandani wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, hata hivyo, korti Malindi akiwa pamoja na watuhumiwa wenza, waliachiliwa bila dhamana yoyote.

Mei 2023, Pauline aliteuliwa kuwa Katibu Msaidizi Masuala ya Mikakati katika chama cha Jubilee.

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Gachagua mswada ukilenga kuzima ‘ajira kwa wenye...

Jeraha la paja kumweka De Bruyne mkekani kwa miezi minne

T L