• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
BORESHA AFYA YAKO: Mbaazi ni mlo mtamu wenye faida tele kwa afya ya binadamu

BORESHA AFYA YAKO: Mbaazi ni mlo mtamu wenye faida tele kwa afya ya binadamu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MBAAZI zimekuwa zikikuzwa na kuliwa katika nchi za Mashariki ya Kati kwa maelfu ya miaka.

Kama chanzo kikubwa cha vitamini, madini, na nyuzinyuzi, mbaazi zinaweza kutoa faida mbalimbali za kiafya kama vile kusaidia kudhibiti uzito, kuboresha usagaji chakula, na kupunguza hatari yako ya kupata magonjwa.

Zaidi ya hayo, mboga hii ya jamii ya kunde ina protini nyingi na hufanya mbadala mzuri wa nyama katika vyakula vingi vya mbogamboga.

Imejaa virutubisho

Mbaazi zina sifa ya lishe bora. Zina idadi ya wastani ya kalori na vitamini na madini kadhaa. Pia ni chanzo kizuri cha nyuzi na protini bila kusahau madini ya manganesi na folati na vitamini B.

Ukila mbaazi unajihisi umeshiba kwa muda mrefu

Protini na nyuzinyuzi kwenye mbaazi zinaweza kusaidia kudhibiti hamu yako ya kutaka kula.

Protini na nyuzi hufanya kazi pamoja ili kupunguza muda wa usagaji chakula, hali ambayo hukufanya kuhisi umeshiba kwa muda. Kwa kuongeza, protini zinaweza kuongeza viwango vya homoni za kupunguza hamu ya kula katika mwili wako.

Chanzo kizuri cha protini ya mmea

Mbaazi ni chanzo kikubwa cha protini ya mimea, hivyo ni chakula bora kwa watu ambao hawali nyama au bidhaa zitokanazo na mifugo au wanyama. Protini aina hii hujulikana kwa jukumu lake katika kudhibiti uzito, afya ya mfupa, na nguvu ya misuli.

Mbaazi zinaweza kukusaidia kudhibiti uzito wako

Mbaazi zinaweza kusaidia kudhibiti uzito ukitegemea ile athari ya kukushibisha kwa muda. Protini na nyuzinyuzi kwenye mbaazi zinaweza kupunguza hamu yako ya kula, jambo ambalo linaweza kupunguza ulaji wako wa kalori wakati wa maankuli.

Inaweza kusaidia udhibiti wa sukari ya damu

Mbaazi zinaweza kusaidia kudhibiti viwango vya sukari ya damu kwa njia kadhaa ikizingatiwa ziko kwenye kategoria ya vyakula vya kiwango cha chini cha glycemic. Pia nyuzinyuzi na protini kwenye mbaazi zinaweza kusaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu. Hii ni kwa sababu nyuzinyuzi hupunguza unyonyaji wa wanga ili kukuza kupanda kwa kasi kwa viwango vya sukari ya damu badala ya kuongezeka. Kula vyakula vyenye protini nyingi kunaweza pia kusaidia kudumisha viwango vya sukari ya damu.

Mmeng’enyo wa chakula

Mbaazi zimejaa nyuzinyuzi ambazo zina faida kadhaa kwa afya kuanzia kwa usagaji chakula.

Nyuzi katika mbaazi kwa kiasi kikubwa huyeyuka, kumaanisha kwamba huchanganyika na maji ili kuunda dutu inayofanana na jeli kwenye njia yako ya usagaji chakula.

Nyuzi mumunyifu zinaweza kusaidia kuongeza idadi ya bakteria yenye afya kwenye utumbo wako na kuzuia kuzidi kwa bakteria hatari kwa afya. Hii inaweza kusababisha kupunguzwa kwa hatari ya hali fulani za usagaji chakula.

  • Tags

You can share this post!

Haaland aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao UEFA baada ya...

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa tosti ya viazi vitamu na...

T L