• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
DOMO: Ni kweli hana haya

DOMO: Ni kweli hana haya

NA MWANAMIPASHO

KASEMA mwenyewe, “nina kila kitu, nisicho nacho ni haya tu.”

Ni maneno yake Seneta Maalum Karen Nyamu.

Sikatai. Kama sura, anayo, kama umbo, alikuwa nalo tena ule mchupa wa Coca-Cola ila sio sasa dada kidogo kajiachilia.

Kama ni hela anazo, kama ni umaarufu anao, kama ni ushawishi wa kisiasa anao, kama ni watoto kajaliwa.Kweli kabisa nakubaliana na lalez Karen, ana vingi vya maana isipokuwa haya.

Lakini vipo vingine asivyo navyo, hana mtu na ndio sababu anakesha kumparamia mume wa mtu.

Taswira anayonichorea mimi huyu lalez, ni ya mwanasiasa soshiolaiti.

Nina uhakika alifanikiwa kuchaguliwa seneta kutokana na baraka za chama cha UDA, isingalikuwa chama, leo angelikuwa akiupunga upepo mkavu kama sisi.

Sielewi ni kwa nini anaendelea kuwa king’ang’anizi katika maisha ya huyo karao.

Bwana mdogo ana mke ila kila kukicha anaishi kumtia aibu na kumdhalilisha Njeri aliyedumu naye kabla hajawa maarufu kupitia sanaa yake ya mugithi.

Karen alimjua karao kutokana na ufanisi kwenye muziki wake. Akajibebisha pale, karao akatizama akaona isiwe tabu kuuma mnofu. Hatua kwa hatua, taratibu akajikuta anachovya asali hadi akazidiwa.Wanasema mchovya asali hachovyi mara moja. Na ndio sababu tayari wana watoto wawili wakati msela yupo kwenye ndoa na mama wa watoto wake kwa zaidi ya miaka 15.

Unapokuwa na mwanamke wa dizaini ya Karen, utahitaji zaidi ya maombi na tembe za usingizi.

Sababu kwa kweli huwa hana haya, hatasita kukuchomea. Hivi kulikuwa na maana gani yeye kwenda kumzodoa huyo Karao wakati akiwa amejistarehesha Dubai na mkewe kwenye kilabu?

Ni vile ana uwezo wa kujilipia ndege ndio sababu aliamua kumfuata karao na mkewe Dubai?

Karen anamchukulia Njeri kuwa mnyonge na ndio sababu anafanya anachokifanya. Anachosahau ni kuwa, Njeri moyoni mwake, anaumia na machungu hayo anayomfanyia.

Wote ni wanawake na ndio kakubali alizaa na mumewe ila kuendelea kumtoneshea moyo kisa ana ushawishi na hela sio sawa.

Mwambieni huyo zimbiting siku karma itakapomwamulia, nayo itamfumania bila haya. Hawa wanawe ambao ni wadogo, watakuja kuwa watu wazima kuona mama yao alivyokuwa akiparamia boma za watu. Na kama atakwepa karma hiyo, basi akumbuke ana watoto. Sasa sijui atakuwa anachekaje au kulia vipi hiyo karma ikimvamia?

You can share this post!

TAHARIRI: KCPE: Serikali itatue lalama kuhusu matokeo

Wasichana pacha wafana katika matokeo ya KCPE

T L