• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Embarambamba: Makabila yote Kenya yananipenda, Kisii pekee ndiyo inanichukia 

Embarambamba: Makabila yote Kenya yananipenda, Kisii pekee ndiyo inanichukia 

NA MERCY KOSKEI

MWIMBAJI wa nyimbo za injili kwa lugha ya Abagusii, Bw Christopher Nyangwara Mosioma maarufu kama Embarambamba amedai kuwa kabila lake la Kisii halimtambui licha ya kuzidi kuendelea kupata umaarufu nchini.

Msanii huyo ambaye ameibuka ni mbinu ya kipekee kutumbuiza mashabiki wake, anasema jamii ya anakotoka – Kisii haimuungi mkono wala kutambua kipaji chake.

Katika mahojiano ya pamoja na baadhi ya ‘wanahabari’ wa makala ya video za You Tube, maarufu kama You Tube content creators kwa Kiingereza, mnamo Septemba 30, 2023, msanii huyo alifichua msururu wa matukio ambayo yamemfanya kuhisi kutothaminiwa katika eneo analotoka.

Embarambamba, anayejulikana kwa uigizaji wake wa ajabu na wa kusisimua jukwaani, alielezea kutamaushwa kwake kutoalikwa kutumbuiza katika hafla zozote Kisii.

Pia, alidai kuwa hapo awali walimkashifu na kumtaja kuwa si wa kawaida alipoanza kazi yake ya usanii.

Mwimbaji huyo, hutumbuiza mashabiki wake kwa kukimbia, kujigaragaza kwenye udongo nyevunyevu na pia kuimba akiwa kwenye mto akioga.

Wakati wa mahojiano na wanakontenti wa You Tube, Embarambamba alisimulia kisa cha kuhuzunisha akidokeza kwamba alioondolewa kwenye orodha ya wanamuziki waliopangwa kutumbuiza katika hafla ya Rais Willia Ruto, Kaunti ya Kisii.

“Sijawahi kutumbuiza kwenye halaiki yoyote Kisii, walinisema vibaya, hata waliniita mwendawazimu na kusema nisihudhurie hafla ya Rais, waliniondoa kwenye orodha ambayo ilikuwa ya kutumbuiza wakati wa ziara ya Rais Ruto Kisii,” Embarambamba alilalamika.

Alidai kuwa makabila yote yamemualika kutumbuiza, ijapokuwa Kisii pekee.

Licha ya malalamishi ya msanii huyo mwenye ukwasi wa ucheshi, ameonekana mara kadha akiwa na mbunge wa Mugirango Kusini, Silvanus Osoro.

Bw Osoro ni mwandani wa Rais Ruto.

Mbunge huyo wa chama tawala cha UDA, 2021 alialika Embarambamba kwenye ofisi yake.

  • Tags

You can share this post!

Masaibu ya afya: Mama asiyeshuhudia hedhi alivyojifungua...

Uhalifu: Kilabu cha burudani Nairobi ambapo simu za walevi...

T L