• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Mkurugenzi wa kampuni ashtakiwa kupora shamba la Jimi Wanjigi

Mkurugenzi wa kampuni ashtakiwa kupora shamba la Jimi Wanjigi

Na Richard Munguti

MKURUGENZI wa kampuni moja jijini Nairobi ameshtakiwa kwa kumpora mwaniaji kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Safina Jimi Wanjigi shamba la thamani ya Sh500 milioni.

Samuel Njuguna Chege mwenye umri wa miaka 53 alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Susan Shitubi.

Chege anadaiwa alishirikiana na watu wengine tisa akiwemo Msajili wa Ardhi Cattwright Jacob Owino ambaye, Bi Shitubi alielezwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kuzirai akiwa katika kituo cha polisi.

Wakili Paddy Cheloti alimweleza hakimu kwamba mshtakiwa Cattwright hakufika kortini kwa vile aliugua ghafla akiwa korokoro ya polisi na kupelekwa Nairobi Hospital.

Bw Chege, mkurugenzi katika kampuni ya Horrison Hills Limited alikanusha mashtaka 17 dhidi yake.

Chege aliagizwa azuiliwe katika kituo cha polisi hadi leo (Alhamisi Aprili 27, 2023) hakimu ajifahamishe zaidi na faili hiyo kabla ya kutoa uamuzi iwapo atamwachilia kwa dhamana au la.

Chege alikana alitekeleza uhalifu huo mnamo Aprili 5, 2018.

  • Tags

You can share this post!

Eric Omondi anyakwa na polisi Kisumu kwa kuandaa maandamano

Miili 8 yafukuliwa idadi ya walioangamia Shakahola ikigonga...

T L