• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Faida za lozi

Faida za lozi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

LOZI, kwa Kiingereza kama almond iko katika jamii ya njugu na ina virutubisho muhimu zinazohitajika katika mwili wa mwanadamu.

Ni chakula chenye kutia nishati mwilini na akilini.

Kuna aina mbili za lozi; kuna lozi tamu lakini pia kuna lozi chungu. Mara nyingi lozi chungu hutumika katika mambo ya kutengenezea vipodozi, mafuta ya lozi (almond oil) na pia manukato.

Ndani ya lozi kuna vitamini B, kalsiamu, mafuta, chuma, nyuzinyuzi, shaba na fosforasi.

Vitu hivi vinasaidia katika upatikanaji wa haemoglobini na pia husaidia ubongo, mishipa, mifupa, moyo na ini kufanya kazi kwa wepesi kabisa.

Lozi insaidia kupanua na kutia nguvu misuli ya ubongo katika kuongeza fahamu.

Utu uzima wa kiumri

Chukua lozi kiasi na uziloweka katika maji na baadaye utoe ngozi kisha uzisage kwa kutumia blenda. Hii huongeza protini ndani ya mwili na hasa kwa watu wazima. Pia unaweza kutia katika maziwa kabla ya kunywewa lakini ni mzuri kwa watoto. Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia mtu kuimarisha mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kwa wenye umri mkubwa.

Upungufu wa damu

Shaba pamoja na chuma na vitamini hutumika katika mfumo wa haemoglobini ya damu. Kwa hiyo, wenye tatizo la upungufu wa damu wanashauriwa kutumia lozi kwa wingi.

Shida ya usagaji wa chakula

Kwa wale wenye matatizo ya usagaji wa vyakula, ni vizuri kula lozi wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala.

Ukoma

Kwa wale wenye maradhi ya ukoma, wasage lozi iwe laini kisha wajipake pale palipoathirika, na pia kwa wale wenye chunusi.

Lozi kukaangwa

Lozi hukaangwa kidogo na huliwa kwa kutafunwa kama ilivyo karanga.

Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.

Aghalabu huwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na aina nyingine za njugu.

Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na virutubisho vingine kama vile madini yanayosaidia kuratibu na kuweka sawa mfumo mzima wa mwili.

Kisukari

Lozi pia inasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.

Mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi, humsaidia kuratibu mfumo wake wa damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya damu inakuwa inafanya kazi jinsi ipasavyo.

  • Tags

You can share this post!

JAMVI: Viunzi tele katika jitihada za Ruto kuvumisha UDA

Watu 13 waangamizwa na corona