• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 10:50 AM
Je, unapaswa kuosha uso wako kwa maji baridi?

Je, unapaswa kuosha uso wako kwa maji baridi?

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KUOSHA uso kwa maji baridi huathiri ngozi kwa njia nyingi nzuri.

Kuzuia chunusi, kwa mfano, ni mojawapo ya faida zinazopatikana.

Hiyo ni kwa sababu maji ya moto huondoa mafuta kwenye ngozi. Hii inaweza kusababisha ngozi yako kutoa mafuta zaidi.

Maji baridi yanaweza kufanya kazi nzuri ya kudhibiti viwango vya mafuta. Maji ya moto husababisha mishipa ya damu kutanuka zaidi, na kufanya ngozi yako kuonekana nyekundu.

Ubaya wa kutumia maji baridi

Kuna baadhi ya vikwazo vya kutumia maji baridi kwenye uso wako. Kwa kuwa maji baridi hukaza vinyweleo vyako, bakteria na uchafu unaweza kunaswa na hautafutika kwa urahisi kama vile kutumia maji yenye joto kiasi.

Unapaswa kuosha uso wako kwa maji ya ufufutende kwanza kama njia ya kuondoa vipodozi na uchafu wowote. Kisha, malizia kwa kusuuza kwa maji baridi ili kukaza vinyweleo na kukuza mzunguko wa damu.

Kwa nini maji ya ufufutende yanaweza kuwa bora

Maji ya ufufutende husaidia kufanya vinyweleo vyako kuonekana vidogo, wakati maji baridi hupunguza uvimbe. Hivyo inapendekezwa uoshe uso wako kwa maji ya ufufutende. Maji ya ufufutende ni mazuri kwa aina zote za ngozi, kwani maji ya moto wa joto la vuguvugu huondoa mafuta ya kinga kwenye ngozi yako ambayo husaidia kuhifadhi unyevu.

Kuna hatari ya kuvunja kapilari ndogo chini ya ngozi yako ikiwa unatumia maji ya moto kwenye ngozi yako au kama vile unabadili kutoka maji moto hadi baridi.

Ni mara ngapi unapaswa kuosha uso wako?

Kwa ujumla, unapaswa kuosha uso wako mara mbili kwa siku – asubuhi na usiku. Kuosha sana kunaweza kukausha ngozi yako na kusababisha kuwasha. Tunakusanya kiasi kingi cha bakteria kwenye foronya zetu, kwa hivyo kusafisha haraka asubuhi kabla kupaka mafuta kwenye uso wako ni muhimu. Uoshaji huo wa mchana ni muhimu pia, kwani husaidia kupunguza uvimbe ambao mara nyingi huwa tunapoamka mara ya kwanza. Kuosha uso wakati wa usiku ni muhimu ili kuonda vipodozi na uchafu wowote uliokusanywa wakati wa mchana kutoka kwa ngozi yako.

Ikiwa unataka kuwa na ngozi inayong’aa, jaribu kuosha uso wako kwa maji baridi. Kuna faida nyingi kwa hili, kama vile vinyweleo vilivyoimarishwa, kuzuia chunusi, na uso unaoonekana kuwa laini zaidi.

Unaweza pia kuongea na daktari wa ngozi au mtaalamu mwingine wa utunzaji wa ngozi ili kujua ni nini kinachofaa zaidi kwa mahitaji yako ya kibinafsi.

  • Tags

You can share this post!

Msichana aliyepata alama 405 KCPE atafuta karo kwa kuvunja...

UJASIRIAMALI: Ufugaji sungura wenye tija

T L