• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
JIJUE DADA: Jinsi ya kukabiliana na mafuta kiunoni

JIJUE DADA: Jinsi ya kukabiliana na mafuta kiunoni

NA PAULINE ONGAJI

MABINTI wengi hukumbwa na changamoto ya kukabiliana na mafuta katika sehemu ya tumbo.

Ni hali ambayo huwa mbaya zaidi mwanamke akishazaa au akitimu umri fulani.

Hali hii hutokana na mkusanyiko wa mafuta yanayozingira viungo vilivyo sehemu ya tumbo na chini ya ngozi.

Ikiwa mzingo wa tumbo lako ni inchi 35 na zaidi, basi uko katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo yanayosababishwa na mafuta hayo.

Changamoto hii imewasukuma wengi kutumia baadhi ya mbinu na taratibu ambazo mara nyingi huwa ni hatari na zina madhara kwa afya.

Badala ya kujihusisha na mbinu hizi hatari, unashauriwa kwamba njia nzuri ya kudhibiti shida hii ni kwa kupunguza kiwango cha kalori unachokula, lakini kabla ya kuchagua lishe inayokufaa wakati huu, tafuta ushauri wa mtaalamu wa lishe.

Baadhi ya vyakula vya kula wakati huu ni kama vile mtindi, tikitimaji, mayai, dengu, pilipili chungu na sukuma wiki.

Lakini pia ili kutimiza ndoto ya kupunguza tumbo, sharti uwe thabiti katika kuzingatia mazoezi.

Hii inamaanisha kwamba unapaswa kuchagua mpango wa lishe bora na kuhakikisha unafanya mazoezi yanayofaa sehemu hii, na uwe na mkufunzi wa mazoezi atakayekusaidia kutimiza ndoto yako.

Ni rahisi kukumbwa na majaribu ya kufanya mazoezi ya kupunguza uzani haraka, lakini unapaswa kukumbuka kwamba mara nyingi mbinu zinazotumika hapa sio za kiafya na haziwezi dhibitiwa na pindi baada ya uzani huo kuisha, kumaanisha kwamba kuna hatari ya sehemu hii kunenepa tena.

You can share this post!

Abdulswamad Nassir aibuka mshindi katika uchaguzi wa...

BORESHA AFYA: Kwa nini ule nyama?

T L