• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 5:50 AM
Kampuni yazindua vitafunio vilivyosindikwa kwa nyama ya kuku

Kampuni yazindua vitafunio vilivyosindikwa kwa nyama ya kuku

NA SAMMY WAWERU

KAMPUNI moja inayoshughulika na masuala ya utotoaji na uanguaji mayai imezindua vitafunio vilivyotengenezwa kwa nyama za kuku.

Kulingana na Kenchic Ltd, vitafunio hivyo vimesindikwa kiasi cha kurahisisha shughuli za mapishi.

Vinajumuisha: crispy kuku nuggets, bites, strip na burger patty, kampuni hiyo ikihoji ni vitafunio mbadala kufuatia ongezeko la bei ya chakula.

Kenchic imesema ubunifu wa bidhaa hizo unalenga kubadilisha dhana ya kuku, kubuni nafasi tele kuvutia wateja kushabikia ulaji wa nyama za ndege hao wa nyumbani.

“Vitafunio tulivyozindua ni vya bei nafuu na rahisi kupika. Ni bora hasa kipindi hiki wakati ambapo gharama ya chakula ni ghali, familia zikihitaji chakula kilichoafikia virutubisho faafu,” akasema Bw Jim Tozer, Mkurugenzi Mkuu Kenchic Ltd.

Mkurugenzi Mkuu Kenchic Ltd, Bw Jim Tozer adokeza kampuni hiyo imezindua vitafunio vya nyama ya kuku. PICHA | SAMMY WAWERU

Uzinduzi wa bidhaa hizo za kula umejiri wakati ambapo Wakenya wameanza kukumbatia ulaji wa kuku, ikizingatiwa kuwa nyama zake ni nyeupe na hazina Cholesterol.

Aidha, Cholesterol ni chembechembe za mafuta ambayo yakikusanyika mwilini yanakuwa hatari kwa afya ya binadamu.

Mafuta hayo yanahusishwa na maradhi ya afya kama vile; Moyo, Pumu na Afkani.

Kilo moja ya nyama za ng’ombe, kondoo na mbuzi imepiku ya kuku, baadhi ya maeneo ile ya kuku wa kienyeji walioimarishwa ikichezea Sh500.

Kwa mujibu wa Kenchic, uzinduzi wa vitafunio hivyo umejiri kufuatia utafiti wa kampuni hiyo unaoonyesha mabadiliko katika mtindo wa kula.

Utafiti huo aidha unaonyesha vijana wanakwepa kushiriki chakula cha pamoja na familia kinyume na mila, itikadi na desturi, wakienda kusaka vyakula vya kisasa.

Miaka ya awali, chakula kilikuwa kile kimoja siku nenda siku rudi pasi yeyote kulalamika, afafanua Bw Tozer, akiongeza kwamba chaguzi la mtindo wa mlo limekengeusha vijana kusaka vyakula vya kisasa.

Ni kufuatia mtazamo huo, afisa huyo anahoji washirika katika mtandao wa uzalishaji chakula wanapaswa kutathmini bidhaa wanazosindika na kujumuisha zinazoshabikiwa na vijana.

  • Tags

You can share this post!

Kafyu Baringo, Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet...

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu mlezi wa vipaji vya watoto

T L