• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Kanisa waumini hushiriki ngono Nairobi baada ya kulishwa chakula cha kiroho lafichuliwa

Kanisa waumini hushiriki ngono Nairobi baada ya kulishwa chakula cha kiroho lafichuliwa

Na MWANGI MUIRURI

IMEBAINIKA kwamba kanisa ambalo washirika huvua nguo na kubakia uchi wa mnyama, kisha kuanza kujamiiana baada ya kulishwa chakula cha kiroho liko katika mtaa wa Uthiru, Kaunti ya Nairobi.

Mbunge wa Maragua Bi Mary wa Maua mnamo Juni 18, 2023 akiwa katika kanisa la PEFA lililoko katika mtaa wa Kamahuha, Kaunti ya Murang’a ndiye alifichua kulihusu.

Uchunguzi wa Taifa Leo Dijitali umebainisha kwamba wachungaji watano wa kanisa hilo tayari wameshurutishwa na maafisa wa kiusalama kuandikisha taarifa huku uchunguzi ukiendelea.

Kanisa hilo limeorodheshwa kama la Pasta anayefahamika kwa jina Mwaura na ambalo limejengwa katika shamba lake binafsi.

Bi Wa Maua alisema kwamba “ikifika tu saa nane, waumini wote bila kujali jinsia na umri huvua nguo na kuanza kushiriki ngono bila kinga yoyote”.

Hivi majuzi, mwanablogu Martha Mwihaki Hinga ambaye hutekeleza ukachero dhidi ya wahaini ndani ya injili alianika kanisa hilo akisema kwamba “huwa na kauli mbio kwamba hakuna tunda la mtu binafsi dunia hii, na kwamba kila mtu hubeba lake kwa niaba ya mwenzake.

Kanisa la ngono

Taarifa zilizoanikwa na Bi Hinga zilifichua kwamba kanisa hilo liko na matawi katika Kaunti za Nakuru, Kajiado, Kiambu na Murang’a na ambapo wengi hujitokeza kwa ibada mwendo wa saa saba na nusu ili wajumuike katika awamu ya ngono kanisani.

“Huku hakuna kujificha wala kujikinga. Wale wa ushoga na wa usagaji kwa pamoja na wake kwa waume hujivinjari kwa ngono bila wasiwasi,” akaandika mmoja wa makachero wa Bi Hinga, akidai kwamba nduguye ni mmoja wa mapasta katika kanisa hilo.

Bi Wa Maua alilitaja kanisa hilo kama Jehanamu huku Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki aliyehudhuria ibada katika kanisa hilo akiapa kudhibiti imani za kiroho nchini kupitia sheria kushinikiza makanisa na wachungaji kupigwa msasa na kusajiliwa.

Profesa Kindiki alisema kwamba “wachungaji wa aina hiyo ni wakora wa kawaida na ni lazima waajibishwe mkondo wa kisheria ili waadhibiwe”.

Bi wa Maua alisema siku hizi kuna makanisa ya vipindi vya kila aina “mimi nikishangaa jinsi inavyoweza kuwa iwapo katika kanisa hili tutapata amri ya tuvue nguo zetu na tuanzane hapa”.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Zari Hassan alenga kupata mtoto wa sita

Waziri Kuria kikaangoni kwa matamshi yake kuhusu shirika la...

T L