• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
KIGODA CHA PWANI: Matarajio ya Wapwani kisiasa mwaka mpya unapoanza leo

KIGODA CHA PWANI: Matarajio ya Wapwani kisiasa mwaka mpya unapoanza leo

Mvutano

“Kuundwa kwa chama kipya kutoka Pwani kitaleta mvutano. Mvutano huu baina ya chama cha Pamoja African Alliance(PAA) na chama hiki kipya kitaleta mgawanyiko katika kura za Pwani. Kitaishia kuzuia chama cha UDA, kupata kura zote za Pwani,” anahoji Bi Mwidau.

Kwa wachambuzi hawa wenye ufahamu mzuri wa siasa za ukanda wa Pwani, mwaka wa 2023 utakuwa nafasi murwa ya kaunti za Pwani kujiwezesha kiuchumi.

“Tunapoingia katika mwaka mpya, ni fursa nzuri ya viongozi wetu kutafuta kujiondoa katika kutegemea mataifa ya Dola kusuluhisha shida za hapa na pale. Ni wakati wa kusuluhisha matatizo yetu kama vile ukosefu wa chakula,” anasema Bw Jenje.

Mwaka mpya unapoanza hii leo, Wapwani wana imani kuwa viongozi wao watawafikiria wanapofanya maamuzi licha ya msemo mwanasiasa ni mwanasiasa.

Ni mwaka wa kuangalia karata ya siasa inavyochezwa na iwapo, itawafaidi wa Pwani au kuzidi kuwaacha katika njia panda kwa manufaa ya wanasiasa.

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA WIKI: Toleo Nambari 18 | Januari 01, 2023

Ajenti ashtakiwa kwa kumtapeli mama mwenye mtoto anayeugua...

T L