• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
KIKOLEZO: Kali za 254 Netflix

KIKOLEZO: Kali za 254 Netflix

NA SINDA MATIKO

TAARIFA za kuwa Country Queen itakuwa Series ya kwanza yenye asili ya Kikenya kupeperushwa kwenye tovuti maarufu ya Kimarekani Netflix, ziligonga vichwa vya habari wiki iliyopita.

Wakenya wengi kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter walionyesha furaha yao kwa hatua hiyo.

Lakini hii sio filamu ya kwanza ya Kikenya kwenye Netflix, tofauti hapa ni kuwa Country Queen itakayoachiwa Julai 15, ni Series.

Ila kuna mizigo mingine ya Kikenya kwenye Netflix ambayo huenda hauifahamu.

Leo nimeamua kuwakusanyia filamu za viwango zenye asili ya Kenya unazoweza pia kushabikia Netflix.

POACHER (2O18)

Ni filamu fupi ya dakika 29 inayohusu uwindaji haramu wa pembe za ndovu. Filamu hiyo ilishutiwa kwenye mbuga ya kitaifa ya Tsavo West.

Poacher ni hadithi ya mkulima mmoja jasiri, anayeamua kuhatarisha maisha yake kwa kuiba pembe za ndovu kutoka kwa wawindaji haramu.

Inakuwa sasa ni zile mbio za paka na panya, wale majangili wanapoamua kumuandama wakiwa na nia ya kuokoa mzigo wao wa kihalifu lakini pia kumwangamiza.

Filamu hii ilifanikiwa kushinda tuzo ya filamu fupi bora kwenye makala ya nane ya tuzo za Kalasha.

PLAN B (2019)

Inawezekana ukawa umeshasikia habari za mzigo huu kutokana na jinsi ulivyotrendi ulipoingizwa sokoni.

Plan B ni drama ya kimapenzi yenye komedi iliyoandaliwa na maprodusa wawili Lowladee aliyeshirikiana na mwigizaji staa, Sarah Hassan.

Kwenye filamu hii, Sarah pia anavalia uhusika wa Lisa Waweru. Baada ya penzi la Ethan (Lenana Kariba) na Lisa kuvunjika, mrembo huyo anaamua kwenda kutoa machungu baa.

Kule anakutana na jamaa asiyemjua (Dela Coker) na wanaishia kuvunja amri ya sita na kwa bahati mbaya Lisa anabeba ujauzito.

Miezi mitano baadaye, anagundua Dela ni jamaa mmoja tajiri na pamoja na rafiki yake, wanapanga mpango wa kumshurutisha aikubali mimba ile ili aweze kutoa matunzo na pia imkwamue Lisa kutokana na hali yake ya msoto.

40 STICKS (2020)

Wahalifu sugu, tisa kati yao wakiwa wamehukumiwa kunyongwa, wapo safarini wakihamishwa kutoka gereza la kiwango cha chini Maza Minium Prison kupelekwa gereza la kiwango cha juu lenye ulinzi mkali Kivu Maximum Prison.

Basi wanalosafiria linapata ajali mbugani kufuatia hali mbaya ya anga na mvua kubwa. Wale wafungwa wanajikuta wakipambania maisha yao dhidi ya wanyama pori na muuaji ambaye amekuwa akiwafuatilia kwa lengo la kummaliza mmoja mmoja.

THE CAPTAIN OF NAKARA (2012)

Ni filamu ya komedi ambayo ni mwigo wa filamu ya Kijerumani The Captain of Kopenick. Mwizi Muntu (Bernard Safari) kaachiliwa kutoka gerezani baada ya kuhudumia kifungo chake.

Muntu anaishia kujipata kwenye penzi nzito na binti wa mhubiri. Kwa kuhofia kuachwa, anaficha historia yake ya uhalifu na badala yake anamwongopea kuwa yeye ni mfanyabiashara tajiri.

Hali hii inamwingiza tena kwenye uhalifu kwani ili kuendelea kuishi uwongo huo pasi na kutambulika, anajikuta akifeki na kudai kuwa ni kapteni wa jeshi la Nakara.

DISCONNECT (2018)

Ni komedi ya kimapenzi inayokuchorea taswira kamili ya jinsi mapenzi mjini Nairobi yalivyo na drama chungu nzima.

Inakupa picha kamili ya wimbo wa Bensoul, Nairobi wenye mshororo maarufu… “Nairobi, yule anayekupea ndio kesho ananiletea, akikula fare…”

Hapa marafiki wawili Celine (Brenda Wairimu) na Josh (Nick Mutuma) na marafiki zao wanajikuta wakikanganywa na maisha ya kimapenzi baina yao na watu wanaowazunguka.

  • Tags

You can share this post!

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola waanza nchini Rwanda

ZARAA: Mfumo wa bustani za PVC unaweza kusaidia raia...

T L