• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:50 AM
ZARAA: Mfumo wa bustani za PVC unaweza kusaidia raia kukabili tatizo la uhaba wa chakula

ZARAA: Mfumo wa bustani za PVC unaweza kusaidia raia kukabili tatizo la uhaba wa chakula

NA SAMMY WAWERU

ATHARI za tabianchi ni bayana, na wataalamu wa masuala ya kilimo wanasisitiza sharti wakulima watathmini mbinu wanazotumia kuendeleza zaraa.

Matumizi ya bustani za paipu za plastiki – PVC – kulingana na John Mutisya, kutoka Biovision Africa Trust ni kati ya mifumo na teknolojia za kisasa kuangazia uhaba wa chakula mijini na maeneo kame.

“Mfumo wa vertical gardens unazuia uvukizi, hivyo basi ni bora katika kilimo endelevu mijini na maeneo kame,” Mutisya asema.

Kaunti 24 zilizoko jangwani na maeneo ya nusujangwa, zinaendelea kuhangaishwa na kero ya kiangazi na ukame, mimea ikikauka na mifugo kufa njaa.

Mutisya anasema vertical gardens, kufuatia muundo wake kudhibiti matumizi ya maji na gharama ya chini ya leba, ndio suluhu ya maeneo yanayopokea kiwango cha chini cha mvua.

Joash Njani na mwanzilishi mwenza wa Urban Smart Gardeners, Pramila Mwibanda wanasema kando na kuhamasisha wakazi mijini kukumbatia bustani za PVC, wanalenga maeneo yenye uhaba wa mvua.

Joash Njani na Pramilla Mwibanda, waanzilishi Urban Smart Gardeners, kampuni inayohamasisha mfumo wa Vertical Gardens kuendeleza kilimo. PICHA | SAMMY WAWERU

“Chini ya majuma manne, mboga zilizopandwa kwa kuzingatia vigezo faafu kitaalamu huwa tayari kuvunwa.”

Vijana hao wanasisitiza mfumo wa vertical gardens unawafaa kwa kiasi kikubwa wamiliki wa ploti na mashamba madogo.

Kupitia matumizi ya bustani za paipu, ni rahisi kukabiliana na wadudu na magonjwa.

Ni mfumo ambao kando na kusaidia kuangazia uhaba wa chakula, mazao yake ni salama kwa kuwa yamezalishwa kwa kutumia mbinuhai.

  • Tags

You can share this post!

KIKOLEZO: Kali za 254 Netflix

Kampuni yakanusha madai ya ubaguzi wa rangi kwa waajiriwa

T L